Pages

Sunday, March 16, 2014

VPL: KAGERA SUGAR 2 v TANZANIA PRISONS 1, SALUM KANONI NA BENJAMINI ASUKIRE WAIPATIA USHINDI KAGERA.

Na Faustine Ruta, Bukoba
Ligi Kuu Vodacom imeendelea leo na Hapa Mjini Bukoba tukishuhudia Timu ya Maafande kutoka Jijini Mbeya imenyukwa bao 2-1 kutoka kwa Kagera Sugar. Kipindi cha kwanza Tanzania Prisons ndio walipata bao kupitia kwa mchezaji wao Peter Michael dakika ya 37 baada ya kuwachambua mabeki wa Kagera Sugar na kuachia shuti kali na kumfunga kipa wa Kagera Sugar. 
Mpaka dakika za mapumziko Tanzania Prisons ndio wameenda kupumzika wakiwa mbele ya Bao 1-0 dhidi ya Wenyeji Kagera Sugar.Kipindi cha pili dakika ya 55 Kagera Sugar walipata penati na mkwaju huo ulipigwa na Salum Kanoni na kupata bao la kusawazisha. Katika dakika za lala salama dakika ya 88 Kagera Sugar walipata bao la ushindi lililofungwa na Benjamini Asukire kwa shuti kali ndani ya eneo hatari la penati nakufanikisha Timu yao kuibuka na ushindi wa bao hizo mbili.
Kikosi Cha Timu ya Tanzania Prisons kilichoanzaWaamuzi wa Mtanange huu wa Kagera Sugar na Tanzania Prisons ya jijini Mbeya
Kipute kimeanza kipindi cha kwanza...
Kipindi cha kwanza hivi ndivyo viongozi wa Kagera Sugar walivyotoka, wakienda Mapumziko wakiwa nyuma ya 1-0.Dakika ya 55 kipindi cha pili Kagera Sugar walipata bao kupitia mkwaju wa penati
Kipa wa Tanzania Prisons hakuna ndani...akifungwa na Salum Kanoni
Mchezaji wa Kagera Sugar Benjamini akitaka kumtoka mchezaji wa Prisons
Patashika zikiendelea uwanjani Kaitaba
Mashambulizi kwenye lango la Kagera yakiondoshwa!!
Patashika wachezaji wa Tanzania Prisons wakimzunguka mwamuzi kwa kile walichoona kwamba mchezaji wao kakwatuliwa ndani ya box na mwamuzi akipinga kwamba ni nje ya box!
.....ni ndani ya box refa!!
Keleleni zote na patashika zikaishia kwenye kupigwa frii kiki
Weka kizuizi hapo!! Kipa akiwapanga wachezaji wake...
Wachezaji wa Kagera Sugar wakipongezana kipindi cha pili baada ya mwenzao Benjamini kupata bao la pili
Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, David Mwamwaja hoi baada ya kupigwa bao la pili!!
Mchezaji wa Kagera Sugar Benjamini Asukire akishangilia bao lake!
Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Jackson Mayanja ambaye ni raia waUganda akiwaelekeza wachezaji wake baada ya timu hiyo kupata bao la pili.
Dakika za nyongeza zikamalizika, Na hapa ni Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Jackson Mayanja akishangilia Ushindi kwa timu yake Kagera Sugar
Yes Yes yes yes yeeees!!!!!! Ni Furaha za Kocha Jackson Mayanja
Aliyeipatia bao la ushindi kagera nae kwenye Kamera!! ni Benjamini Asukire(kulia)
Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, David Mwamwaja akitoa lawama kwa Mwamuzi baada ya mpira kumalizika!!!

No comments:

Post a Comment