Pages

Friday, March 28, 2014

UTATA WAIBUKA FIFA KUFUATIA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA YA MWAKA 2022 KUCHEZWA HUKO QATAR


Michel Platini, rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA.Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, Michel Platini , amemuunga mkono rais wa taasisi ya uchunguzi ya shirikisho la soka duniani FIFA, Michael Garcia. Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Uingereza utafiti uliyofanywa na Garcia juu ya michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2022 huenda hakufurahisha baadhi ya wanachama wa shirikisho la soka duniani FIFA.
"Ninalani jitihada zote ziliyofanywa ili kuzuia zoezi la uchunguzi huu, ni lazima uchunguzi huu ukamilike," amesema Platini katika tangazo alilokabidhi AFP.
Michael Garcia, mwendesha mashtaka wa zamani katika mji wa New York, anaendesha uchunguzi juu ya masharti yaliyotumiwa kwa kuamua desemba 2010 michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2022 ichezwe nchini Qatar ( na michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2018 ichezwe nchini Russia), hali ambayo imezua utata.
Vyombo vya habari nchini Uingereza vilifahamisha mapema wiki hii kwamba baadhi ya wajumbe wa Fifa walikuwa tayari kuhojiwa na Garcia, huku baadhi ya wajumbe hao wakifikiri, hata yale ambayo hayajatekelezwa, hali ambayo imezua fujo na kuongeza mgogoro wa maslahi. Garcia ni raia kutoka Marekani wakati taifa hilo lilikuwa mgombea kwa maandalizi ya kombe la dunia mwaka 2022.
Gazeti la Daily Telegraph lilichapisha habari wiki iliyopita kwamba lina nyaraka zinazoonyesha kwamba Jack Warner , ambaye alikuwa makamu wa rais wa FIFA wakati wa kura juu ya michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2022, pamoja na wanachama wa familia yake wanadaiwa kupokea takriban euro milioni 1.43 kutoka kampuni inayomilikiwa na raia wa Qatar, Mohamed Bin Hammam , ambaye wakati huo, alikua rais wa shirikisho la soka barani Asia .

Watu wawili ambao walikuwa wakituhumiwa kujaribu kununua kura katika kipindi cha pili cha uchaguzi, kwa kugombea urais wa FIFA katika mwaka 2011 ili hali si wajumbe tena katika shirikisho la soka duniani.

No comments:

Post a Comment