
Michel Platini, rais wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA.
Rais
wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, Michel Platini , amemuunga
mkono rais wa taasisi ya uchunguzi ya shirikisho la soka duniani FIFA,
Michael Garcia. Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Uingereza utafiti
uliyofanywa na Garcia juu ya michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2022
huenda hakufurahisha baadhi ya wanachama wa shirikisho la soka duniani
FIFA.
"Ninalani
jitihada zote ziliyofanywa ili kuzuia zoezi la uchunguzi huu, ni lazima
uchunguzi huu ukamilike," amesema Platini katika tangazo alilokabidhi
AFP.
Michael
Garcia, mwendesha mashtaka wa zamani katika mji wa New York, anaendesha
uchunguzi juu ya masharti yaliyotumiwa kwa kuamua desemba 2010 michuano
ya kombe la dunia ya mwaka 2022 ichezwe nchini Qatar ( na michuano ya
kombe la dunia ya mwaka 2018 ichezwe nchini Russia), hali ambayo imezua
utata.
Vyombo
vya habari nchini Uingereza vilifahamisha mapema wiki hii kwamba baadhi
ya wajumbe wa Fifa walikuwa tayari kuhojiwa na Garcia, huku baadhi ya
wajumbe hao wakifikiri, hata yale ambayo hayajatekelezwa, hali ambayo
imezua fujo na kuongeza mgogoro wa maslahi. Garcia ni raia kutoka
Marekani wakati taifa hilo lilikuwa mgombea kwa maandalizi ya kombe la
dunia mwaka 2022.
Gazeti
la Daily Telegraph lilichapisha habari wiki iliyopita kwamba lina
nyaraka zinazoonyesha kwamba Jack Warner , ambaye alikuwa makamu wa rais
wa FIFA wakati wa kura juu ya michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2022,
pamoja na wanachama wa familia yake wanadaiwa kupokea takriban euro
milioni 1.43 kutoka kampuni inayomilikiwa na raia wa Qatar, Mohamed Bin
Hammam , ambaye wakati huo, alikua rais wa shirikisho la soka barani
Asia .
Watu wawili ambao walikuwa wakituhumiwa
kujaribu kununua kura katika kipindi cha pili cha uchaguzi, kwa kugombea
urais wa FIFA katika mwaka 2011 ili hali si wajumbe tena katika
shirikisho la soka duniani.
Post a Comment