Pages

Wednesday, March 12, 2014

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: BAYERN MUNICH 1 v ARSENAL 1, (Agg 3-1) SARE YAWATUPA NJE GUNNERS ALLIANZ ARENA! BASTIAN SCHWEINSTEIGER AKITUPIA NA LUKAS PODOLSKI AKISAWAZISHA BAO HILO.

Bastian Schweinsteiger akishangilia bao lake kipindi cha pili.Wachezaji wa Bayern wakipongezana baada ya kupata baoLukas Podolski nae baada ya dakika mbili akishangilia kwa kusawazisha!!Nipe tano ndugu yangu!!Wamerudishaje !!Pamoja na Bayern kufanya mashambulizi ya hapa na pale mtanange unafikia hatua ya mapumziko timu zote mbili zikiwa bado ziko 0-0, Hakuna aliyeweza kuziona nyavu za mwenzake. Kipindi cha pili dakika ya 55 Bastian Schweinsteiger anaipachikia bao kiurahisi akiwa ndani ya box baada ya kupata pasi kutoka kwa Franck Ribéry. Dakika mbili baadae Lukas Podolski alimsukuma mchezaji wa Bayern Munich kwenye eneo hatari la penati na Mwamuzi kudai kupute kiendelee kwa kupeta na hatimae Lukas Podolski kuachia shuti kali na kumfunga kipa wa Bayern Munich na kusawazisha kwa kufanya 1-1.Dakika ya 59 Bayern wanafanya mabadiliko Mario Götze anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Toni Kroos. Dakika za majeruhi dakika ya 90 Thomas Müller anakosa penati..Kipa wa Arsenal Lukasz Fabianski anaudaka. Mpira unamalizika kwa Matokeo ya 1-1 na Arsenal wanaondoka kwenye mashindano haya ya UEFA Champions Ligi kwa Agg. ya 3-1 baada ya kutoshana nguvu leo kwa bao 1-1 kwenye marudiano, Ambapo mechi ya kwanza Arsenal walifungwa bao 2-0 huko Emirates. Kipa wa Bayern Munich akiokoa mpira ulipigwa kwa kichwa na Olivier Giround ndani ya lango lake katika kipindi cha kwanza.
Mapema kipindi cha kwanza Javi Martinez frii kiki ilipigwa na kufanikiwa kuifunga Arsenal lakini mwamuzi wa pembeni aliliona kuwa alikuwa kaotea siyo bao...
Mikel Arteta akipewa kadi ya njanoTwendelee!!!Kipa wa Gunners alivyookoa mkwaju wa penati..1-1 wasalimie Arsenal...!Philipp Lahm of Bayern Munich hands over a cheque to the International Committee of the Red Cross (ICRC) prior to his side's clash with ArsenalMapema wakifanya mazoezi Bayern.
VIKOSI:
Bayern Munich:
Neuer, Lahm, Javi Martinez, Dante, Alaba, Robben, Schweinsteiger, Thiago, Ribery, Gotze, Mandzukic.
Subs:
Starke, Van Buyten, Rafinha, Pizarro, Boateng, Muller, Kroos.
Arsenal: Fabianski, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Vermaelen,
Cazorla, Arteta, Oxlade-Chamberlain, Podolski, Ozil, Giroud.
Subs: Viviano, Rosicky, Flamini, Jenkinson, Gnabry, Hayden.
Referee: Svein Oddvar Moen (Norway)

No comments:

Post a Comment