Pages

Friday, March 14, 2014

RAIS WA BAYERN MUNICH AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 3 NA NUSU KWA KUKWEPA KODI

Rais wa Bayern Munich amehukumiwa kwenda jela kwa kifungo cha miaka mitatu na miezi sita kutokana na kosa la kukwepa kodi.
Uli Hoeness, 62, alikiri kukwepa kodi inayofikia kiasi cha €18.5 million kupitia akaunti zake za benki za siri lakini utetezi wake wa kukiri kosa akidhania ungemsaidia kuepukana na adhabu ya kifungo ulishindwa kumsaidia.
Mwndesha mashtaka alitaka Hoeness afungwe jela miaka mitano na nusu kwa kutokana na kupatikana na hatia ya kukwepa kodi.

Mwishowe, jaji wa mahakama iliyokuwa ikisikiliza kesi hiyo akaamuru mwanasoka huyo wa zamani wa Ujerumani Magharibi atumikie kifungo cha miaka 3 na miezi sita.
Happier times: Hoeness shows off the Bundesliga trophy as Bayern parade last seasons' treble to their fans
Uli Hoeness na viongozi wengine wakionesha makombe yao Bundesliga, Msimu uliopita kwa wadau na mashabiki, walishinda makombe matatu(treble). 'We thank you for everything': Bayern fans show their support for the club's president outsideMashabiki wa Bayern Minich wakionesha ujumbe wao, Tunkushukuru kwa kila jambo!

No comments:

Post a Comment