Pages

Friday, March 28, 2014

NSSF MEDIA CUP KUANZA KUTIMUA VUMBI MACHI 29


Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akizungumza wakati swa hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu zinazoshiriki mashindano ya NSSF Media Cup yanayotarajiwa kuanza rasmi Machi 29.

Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akizungumza wakati swa hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu zinazoshiriki mashindano ya NSSF Media Cup yanayotarajiwa kuanza rasmi Machi 29.

Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akimkabidhi vifaa vya michezo, mwakilishi wa timu ya Star Tv, Tom chilala kwa ajili ya mashindano ya NSSF CUP yanayotarajiwa kuanza Machi 29.

Baadhi ya vifaa vilivyotolewa kwa timu shiriki katika michuano ya NSSF Media Cup.

Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (kushoto), akimkabidhi vifaa vya michezo, mwakilishi wa Kampuni ya Free Media Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, Francis Dande kwa ajili ya mashindano ya NSSF MEDIA CUP yanayotarajiwa kuanza Machi 29.


Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (kushoto), akimkabidhi vifaa vya michezo mwikilishi wa Jambo Leo, Julius Kihampa.

Antony Siame, mwakilishi wa gazeti la Raia Mwema akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (kushoto).

Na Mwandishi Wetu
JUMLA ya sh. millioni 19 zimetolewa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ikiwa ni fedha taslimu zitakazotolewa kwa washindi mbalimbali wa michezo ya NSSF MEDIA CUP 2014 itakayoanza Machi 29.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Meneja Kiongozi wa Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika hilo, Eunice Chiume, alisema kuwa maandalizi ya michuano hiyo imekamilika na kwa upande wa mpira wa miguu mshindi wa kwanza atapata Tshs. 4,500,000, mshindi wa pili atapata Tshs.3,500,000 na watatu atapata Tshs. 2,000,000.


Aidha alisema, kwa upande wa mpira wa Pete mshindi wa kwanza atazawadiwaTshs. 4,000,000, mshindi wa pili Tshs.3,500,000 na mshindi wa tatu atazawadiwa Tshs. 2,000,000 taslimu.

No comments:

Post a Comment