Na Mwandishi maalumu, Tukuyu
Wachezani 29 kati ya 34 waliochaguliwa katika programu maalumu ya marekebisho ya timu ya Taifa inayoendeshwa na TFF wameshaanza mazoezi makali katika Wilaya ya Rungwe, Mbeya.
Wachezaji hao, ambao wametokea katika mikoa mabali mbali, waliingia kambini siku ya Jumamosi huku wakiongozwa na Mwalimu Salum Mayanga akisaidiwa na Patrick Mwagata, ambaye ni kocha wa makipa, Meja Joakim Mashanga ambaye ni daktari wa team na Fred Chimela ambaye ni Meneja Vifaa.
Timu ya Taifa, Taifa stars, inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager kwa mwaka wa pili mfululizo sasa, inatarajiwa kupata mabadiliko makubwa sana ndani ya miezi miwili ijayo ili ipatikane timu bora itakayoshiriki katika mechi za kufuzu kupata tiketi ya kucheza Kombe la Afrika.
No comments:
Post a Comment