Manchester
City watatua Emirates kupambana na Kikosi cha Arsene Wenger, Arsenal,
kwenye Mechi muhimu mno katika hatima ya Ubingwa wa Ligi Kuu England
ambapo Mshindi wake atakuwa amejipigia hatua kubwa kwenye mbio za kutwaa
Taji.
Katika Siku za hivi karibuni, Wenger amekuwa na mikosi mikubwa baada kutandikwa 6-0 na Chelsea na kuruhusu Bao, tena la kujifunga wenyewe, walipotoka Sare 2-2 na Swansea City katika Mechi yao iliyofuatia baada ya kipigfo chao kikubwa ambayo walicheza Juzi Jumanne.
Man City wapo Nafasi ya 3, Pointi 3 nyuma ya Chelsea lakini wana Mechi mbili mkononi, na baada ya Jumanne kuitwanga Man United 3-0 Uwanjani kwao Old Trafford, watataka kuendeleza wimbi lao la ushindi kwa pia kuifunga Arsenal.
Wakati Chelsea Wikiendi watasafiri kwenda kucheza na Timu inayosuasua Crystal Palace, Liverpool, ambao wapo Nafasi ya Pili, Pointi 1 nyuma ya Chelsea, wapo Nyumbani Anfield kuikaribisha Tottenham Hotspur, Timu isiyotabirika.
Akiongelea Mechi yao na Man City, Wenger amesema: “City walipata ushindi mzuri na United, wanaonyesha hawawezi kuzuilika na wao ndio wenye nafasi kubwa ya kutwaa Ubingwa kwani wana Mechi mbili mkononi. Wao na Chelsea ndio wana nafasi kubwa! Sisi nafasi yetu finyu kwani inabidi tusikosee hata kidogo!”
Lakini Nahodha wa Man City, Vincent Kompany, ambae Timu yake iliitandika Arsenal Bao 6-3 katika Mechi yao ya Ligi Msimu huu huko Etihad, amesema Mechi hii ni ngumu.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
Jumamosi Machi 29
15:45 Man Utd v Aston Villa
18:00 Crystal Palace v Chelsea
18:00 Southampton v Newcastle
18:00 Stoke v Hull
18:00 Swansea v Norwich
18:00 West Brom v Cardiff
20:30 Arsenal v Man City
Jumapili Machi 30
15:30 Fulham v Everton
18:00 Liverpool v Tottenham
Jumatatu Machi 31
22:00 Sunderland v West Ham

No comments:
Post a Comment