Meneja wa kinywaji cha Redd’s Origina Victoria kimaro katikati akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wa viongozi wa kamati ya Miss Tanzania katika siku ya kufunga semina ya mawakala wa shindano la Redd’s miss Tanzania kwa mwaka huu, kushoto kwake ni mkurugenzi wa kampuni ya LINO Intenational Agency Hashim Lundenga, Redd’s Miss Tz 2013 Happines Watimanya na Meneja masoko wa TBL Vimal Vaghmaria kulia mwenye miwani.
Redd’s Miss Tz 2013 Happines Watimanya akiwa katika picha ya pamoja na mawakala wa shindano la Redd’s miss Tanzania 2013 kwenye semina ya mawakala hao kulia waliokaa ni meneja wa Redd’s Original Victoria kimaro na kushoto ni Meneja masoko wa TBL Vimal Vaghmaria mwenye miwani na wa mwisho ni mkuu wa itifaki wa kamati ya Miss Tanzania Albert makoye.
======== =======
MAWAKALA wanaoandaa mashindano ya urembo hapa nchini ‘Redd’s Miss Tanzania 2014” kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini wametakiwa kutotangaza zawadi kwa washindi ambazo hawana kwa sababu wakifanya hivyo wanashusha heshima ya mashindano hayo imeelezwa jana jijini Dar es Salaam.
Akizungmza jana katika semina ya mawakala hao, Meneja wa bia ya Redd’s Original, Victoria Kimaro, alisema kuwa hali hiyo inawafanya washiriki, wazazi, walezi na wadau wa sanaa hiyo kuzungumzia vibaya sanaa hiyo.
Kimaro aliwataka mawakala hao kuhakikisha wanatangaza zawadi walizokuwa nazo na kuwakumbusha pia kutafuta warembo wenye vigezo vya juu ili baadaye mmoja wao aweze kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi katika fainali za dunia.
“Usiahidi kitu usichokuwa nacho, watu wameahidi vitu vikubwa ambavyo hawajafanikiwa kuvipata mpaka siku ya shindano…sio vizuri na ninawashauri msifanye tena hivyo ili kujenga shindano letu,” alisema meneja huyo wa Redd’s.
Aliwataka mawakala hao pia kufanya mazungumzo na makampuni na taasisi nyingine kwa ajili ya kuomba udhamini wa kusaidia mashindano hayo na si kutegemea wadhamini wakuu peke yao ambao wanhitaji kusimamia fainali za taifa kikamilifu.
“Tujipange kufanya maandalii yaliyo bora…kama Redd’s tutajaribu kufika kila mahali kwa uwezo wetu ila nawasisitiza na kuwakumbusha tafuteni mbinu za kuuza mashindano yenu,” aliongeza Kimaro.
Naye Mshauri wa Ufundi wa Kamati ya Redd’s Miss Tanzania, Ramesh Shah, aliwataka mawakala hao kuwaandaa vizuri washiriki kwa sababu wengi wao wanakuwa ni wahitimu wa elimu ya Sekondari hivyo wanahitaji mwongozo.
Aliwataka mawakala hao kuthamini sanaa hiyo ya urembo kwa sababu ni moja ya michezo inayosaidia kukuza uchumi na kutangaza jina la nchi katika ngazi mbalimbali.
Redd’s Original ndiyo wadhamini wakuu wa shindano hilo kwa mwaka watatu mfululizo na mwaka huu wanatarajiwa kutumia zaidi ya Sh. Milioni 500….
No comments:
Post a Comment