Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, March 28, 2014

MANCHESTER CITY WAIPANIA ARSENAL JUMAMOSI.

Manchester City watatua Emirates kupambana na Kikosi cha Arsene Wenger, Arsenal, kwenye Mechi muhimu mno katika hatima ya Ubingwa wa Ligi Kuu England ambapo Mshindi wake atakuwa amejipigia hatua kubwa kwenye mbio za kutwaa Taji.
Katika Siku za hivi karibuni, Wenger amekuwa na mikosi mikubwa baada kutandikwa 6-0 na Chelsea na kuruhusu Bao, tena la kujifunga wenyewe, walipotoka Sare 2-2 na Swansea City katika Mechi yao iliyofuatia baada ya kipigfo chao kikubwa ambayo walicheza Juzi Jumanne.

Man City wapo Nafasi ya 3, Pointi 3 nyuma ya Chelsea lakini wana Mechi mbili mkononi, na baada ya Jumanne kuitwanga Man United 3-0 Uwanjani kwao Old Trafford, watataka kuendeleza wimbi lao la ushindi kwa pia kuifunga Arsenal.

Wakati Chelsea Wikiendi watasafiri kwenda kucheza na Timu inayosuasua Crystal Palace, Liverpool, ambao wapo Nafasi ya Pili, Pointi 1 nyuma ya Chelsea, wapo Nyumbani Anfield kuikaribisha Tottenham Hotspur, Timu isiyotabirika.

Akiongelea Mechi yao na Man City, Wenger amesema: “City walipata ushindi mzuri na United, wanaonyesha hawawezi kuzuilika na wao ndio wenye nafasi kubwa ya kutwaa Ubingwa kwani wana Mechi mbili mkononi. Wao na Chelsea ndio wana nafasi kubwa! Sisi nafasi yetu finyu kwani inabidi tusikosee hata kidogo!”

Lakini Nahodha wa Man City, Vincent Kompany, ambae Timu yake iliitandika Arsenal Bao 6-3 katika Mechi yao ya Ligi Msimu huu huko Etihad, amesema Mechi hii ni ngumu.

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA

Jumamosi Machi 29

15:45 Man Utd v Aston Villa

18:00 Crystal Palace v Chelsea

18:00 Southampton v Newcastle

18:00 Stoke v Hull

18:00 Swansea v Norwich

18:00 West Brom v Cardiff

20:30 Arsenal v Man City


Jumapili Machi 30

15:30 Fulham v Everton

18:00 Liverpool v Tottenham


Jumatatu Machi 31

22:00 Sunderland v West Ham

No comments:

Post a Comment