Pages

Tuesday, March 11, 2014

CPWAA KUANZA KUGAWANA MAPATO NA MAPRODUCERS!

Msanii wa muziki wa Kizazi kipya Ilunga Khalifa a.k.a CPwaa kuanza rasmi utaratibu wa kugawana mirabaa na watengenezaji na wasimamizi wa kazi zake za sanaa. 
Maamuzi haya yamekuja chini ya mkataba mpya ambao CPwaa ameingia na “Record label” yake ya “Brainstormusic” ambayo itazinduliwa rasmi siku za usoni.Maamuzi haya ni magumu kwa wasanii wengi lakini kwa wale wafuatiliaji na wadau wa muziki hakika wanatambua biashara ya muziki inafanyikaje na jinsi kila muhusika anavyotakiwa kupata share zake kutokana na makubaliano yaliyofikiwa na pande zote kupitia sheria za kitaifa na kimataifa za haki miliki.

CPwaa ambaye amakuwa akifanya kazi na “Brainstormusic” kwa miaka mingi tayari amekuwa na mafanikio makubwa kimuziki kupitia uongozi na usimamizi wa kampuni hiyo.Ukiacha tuzo 3 za Kilimanjaro Muisc awards,nomination za tuzo za kimataifa kama Channel O ,CPwaa anaendelea kufaidika kupitia mikataba mizuri ya shows na endorsements kwenye makampuni mbalimbali kupitia label hiyo. 

..”Kupitia Brainstormusic nimejifunza vitu vingi sana kuhusu sanaa ya muziki baadaa kufanya kazi na makampuni ya hapa Tanzania na nje.Nimesafiri nchi nyingi Africa na Asia kupitia muziki na kusema ukweli Tanzania kuna mambo mengi sana bado hayako sawa kwenye biashara ya muziki” Umefika muda wa sasa kushare experience na knowledge na kama tukifata utaratibu huu hakuna mtu atadhulumiwa wala kulalamika.Kila mdau anahusika.”…..aliongezea CPwaa!! 

Kwenye utayarishaji wa muziki kila muhusika huwa anakuwa kiwango fulani cha asilimia ya mapato anapata kutokana na mchango wake.Kwa kawaida mapato ya muziki “Royalties” hugawanywa kati ya Songwriter ( mtunzi wa nyimbo ambae ndio mmliki halali wa nyimbo), Producer ( Mtayarishaji), Performing Artist ( Muimbaji wa nyimbo) na Publisher au Record label ( wasambazaji na wasimamizi). Mgawanyo unatokana na kiwango cha mchango wa kila muhusika na mara nyingi huwa makubaliano kati ya wahusika. Kimataifa au kawaida mtunzi huchukua asilimia kubwa na wengine hupata sehemu tu mirabaa itakayokusanywa.Serikali haihusiki na makubaliano ya asilimia za mirabaa kati ya wahusika au hatua za awali za hiyo sanaa ila inahusika kwenye kuweka na kutoza kiwango fulani kinacholipwa na vyombo vyote vinavyotumia kazi za sanaa na kisha kugawa mirabaa kwa wale wamiliki wa hizo sanaa. 

Kuanzia mwaka huu Producer yeyote atakayefanya kazi na CPwaa chini ya usimamizi wa “Brainstormusic” basi atafaidika si tu kwenye malipo ya awali ya utengenezaji wa beat na studio time ila pia asilimia fulani ya mapatao ya mirabaa itakayoingizwa na kazi hiyo. Kimataifa producer huchukua kati ya 20 – 25% kutokana na kwamba yeye kama mtengenezaji wa beat basi ndio mmliki wa ile beat. 

Huu ni utaratibu mpya utakuwepo kwa maproducer wote watakaofanya kazi na CPwaa au Brainstormusic kuanzia mwaka huu: 

1.Kazi zote zitaandaliwa na kufanywa chini ya makubaliano yaliyoandikwa na kusainiwa na pande zote.Invoice na risiti zitahusika. 

2.Brainstormusic ikinunua beat pamoja na haki miliki zake ( yaani producer akiuza beat jumla) basi hatapata share za mirabaa. 

3.Kama Brainstormusic au Msanii wake atahusika kwenye hatua za utayarishaji beat,vionjo,idea,upangiliaji basi asilimia fulani ( Chini ya makubaliano) ya mirabaa itatolewa na Brainstormusic kwa Producer wa kazi hiyo. 

4.Kama producer atahusika mwanzo mwisho kutengeneza na kukamilisha beat hiyo bila uhusika wa Brainstormusic au msanii wake basi producer atapata asilimia fulani kubwa zaidi ( Chini ya makubaliano) ya mapato ya mirabaa ya kazi hiyo. 

5. Ukiacha mapato ya mirabaa Brainstormusic itamlipa Producer au Studio gharama za kawaida ( Delivery / Studio Fee) kama utaratibu ulivyo sasa. 

Brainstormusic ni Record label ya kujitegemea inayofanya kazi na wasanii,maproducers na makampuni mbalimbali.Mwaka huu imedhamiria kujitanua kwenye Music Publishing hivyo kupitia mikataba yake itahakikisha producer analipwa asilimia yake kutoka makampuni mbalimbali kama ikiwemo Music Stores,makampuni ya milio ya simu na PROs ( Performance Rights Organization) kama COSOTA. 

Bado hakuna utaratibu mzuri nchini Tanzania unaotumika kwenye utendaji na usimamizi wa kazi za sanaa kuanzia hatua za awali.”Brainstormusic” tunatambua mchango na kuheshimu kila mtu kwenye “Food Chain” ya sanaa na hivyo tutafanya kazi kufuata miongozo ya kitaifa na kimataifa ambapo kila mtu anapata maslahi kutokana na mchango wake. Utaratibu huu hautaishia kwa CPwaa tu bali wasanii wote watakaokuwa wakisimamiwa na “Brainstormusic”.

Asanteni sana. 
By CPwaa’s Management

No comments:

Post a Comment