CHELSEA 6 v ARSENAL 0, GUNNERS WANYOOSHWA DARAJANI LEO!!! MECHI YA 1000 YA MZEE WENGER YAMALIZIKA KWA MIUJIZA!
Ligi kuu England imeendelea tena leo na kushuhudia mtanange kwenye uwanja wa Stamford Bridge, Arsene Wenger na Timu yake ataiongoza timu yake Arsenal katika Mechi yake ya 1,000 kwa uongozi wa Arsene Wenger kama Meneja wa Klabu hiyo na mtanange kumalizika kwa bao 6-0 dhidi ya Arsenal. Bao zimepatikana katika kipindi cha kwanza na cha pili, Huku bao 4 zikifungwa kipindi cha kwanza na mbili kipindi cha pili.
Samuel Eto'o ndie aliyeanza kuwafungia Chelsea bao la kwanza baada ya kupata mpira kutoka kwa Andre Schürrle Katika dakika ya mapema dakika ya 5, Dakika ya 7 baada ya dakika mbili kupita Andre Schürrle akaongeza bao jingine na kufanya 2-0 baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Nemanja Matić dhidi ya Arsenal inayoongzwa na Arsene Wenger.
Dakika ya 16 mchezaji wa Arsenal Kieran Gibbs akapewa kadi nyekundu baada ya mpira kuunawa kwenye eneo la penati na mwamuzi kudai mpira ni penati na penati hiyo ikafungwa dakika 17 na Eden Hazard. Dakika ya 42 Oscar akawachoma bao jingine la nne na kufanya magoli kuwa 4-0 akipewa pasi na Fernando Torres na mpira kumalizika kwa kipindi cha kwanza wakiwa mbele Chelsea dhidi ya Arsenal kwenye uwanja wa nyumbani Stamford Bridge.
Kipindi cha pili Dakika ya 66 Oscar akawashona bao la tano na kufanya mabao kuwa 5-0 dhidi ya Arsenal. Dakika ya 71 Mohamed Salah akawaongezea bao jingine tena Chelsea na kufanya bao 6-0 baada ya kupewa pasi na Nemanja Matić .
Post a Comment