Pages

Saturday, February 1, 2014

YANGA YAKANUSHA WACHEZAJI WAKE KUPIGANA WAKATI WAKIWA TANGA

Benchi la Ufundi la klabu ya Young Africans limesema limesikitishwa na taarifa zilizoenea kwenye baadhi ya vyombo vya habari kwamba wachezaji wao wawili  kiungo Haruna Niyonzima na nahodha Nadir Haroub "Cannavaro" walipigana katika mchezo dhidi ya Coastal Union siku ya jumatano jijini Tanga na kudai kuwa habari hizo hazina ukweli wowote bali ni katika kutaka kuharibu twasira ya timu.
Taarifa ya klabu hiyo iliyonukuliwa kupitia mtandao wa klabu hiyo ambazo zimemnukuu kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa zimesema kuwa benchi la ufundi limeshangazwa na taarifa hizo baada ya kuziona na kuzisoma hii leo na kusisitiza walioandika wamefanya hivyo kwa ajili ya maslahi yao tu.
Akinukuliwa Mkwasa amesema wameshangazwa na taarifa hizo kwani watu walikuwepo uwanjani na aliweza kushuhudia mchezo huo, hakuna aliyeona Cannavaro na Niyonzima wakipigana katika kipindi chote cha dakika 90 za mchezo, na kwamba washikwa na wasi wasi na waandishi waliokuwepo uwanjani kama walikua makini kufuatilia mchezo na kuandika kitu tofauti na walichokiona.
  
Akizidi kunukuliwa Mkwasa amesema Sheria za soka zipo wazi, mchezaji au wachezaji wapigana ndani ya uwanja mwamuzi anawatoa nje ya uwanja kwa kuwapa kadi nyekundu, sasa wameshangaa kuona taarifa hizo zilizoripotiwa leo kuwa kuna wachezaji wao walipigana huku wachezaji wote wakimaliza dakika 90 za mchezo huo.
Kuhusu maandalizi ya mchezo wa jumapili Mkwasa amesema vijana wake leo wamefanya mazoezi asubuhi kujiandaa na mchezo huo, na hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja kwani Hamis Kiiza, Hassana Dilunga waliokuwa wagonjwa wameshaungana wenzao kambini na Athuman Idd "Chuji"  aliyekua amesimamishwa kurejeshwa kundini.

No comments:

Post a Comment