Pages

Tuesday, February 4, 2014

REKODI MBAYA YA KOCHA DAVID MOYES WA MAN UNITED NDANI YA MIEZI SITA

Imekuwa ngumu sana kwa David Moyes kufuata nyayo za Mscot mwenzie Sir Alex Ferguson ndani ya Manchester united.
Hata hivyo, sio wengi wangeweza kubashiri kuwa Moyes angekuwa na kibarua kigumu kama ilivyo.
Kilicho haribu zaidi, kwa muda mfupi tu tangu atimbe Old Trafford, Club imeshuhudia kuvunjika kwa rekodi lukuki zilizowahi kuwekwa huko nyuma

Hapa chini ni baadhi tu ya rekodi hizo:
1984: Stoke City juzi imepata ushindi wa kwanza kwa United baada ya miaka takribani 30, mara ya mwisho kuifunga United ilikuwa mwaka 1984. 
 
82: Kufungwa na Tottenham Hotspur, Swansea City na Sunderland ina maanisha katika miaka 82 Man U wamepoteza mechi zao 3 za kwanza za kalenda ya mwaka,hii ni tangu 1932.Kipindi hicho,kikosi cha Walter Crickmer kilichapwa na Bradford Park Avenue, Plymouth Argyle na Swansea City 
1974: Kwa mwezi wa Januari tu, United wameshapoteza mechi tatu. Hii haijawahi kutokea tangu mwaka 1974

22: Mechi hizo pia zimepelekea United kupoteza mechi tatu ndani ya wiki moja kwa mara ya kwanza katika misimu 22


2001: Tukibaki hapo hapo kwenye kiwingu cha kupoteza mechi tatu,kwa mara ya mwisho ilitokea miaka 13 iliyopita wakati Derby County, Southampton na Tottenham Hotspur walipoibuka kidedea dhidi ya Mashetani wekundu.


10: Kwa Swansea, wao hawajawahi kushinda katika dimba la Old Trafford kabla ya ushindi wao wa 2-1 kwenye kombe la FA – hii ni katika mechi 10 zilizopita.


20: Sunderland wamevunja mwiko mwaka huu,kwa mara ya kwanza wameichapa United baada ya kujaribu kufanya hivyo kwa mara 20.Kwao ni bonge la ushindi,mara ya mwisho ilikuwa ni kombe la ligi mwaka 2000.


1992: Mwaka ambao Everton – Klabu ya zamani ya Moyes ilishinda Old Trafford kabla ya kampeni hii.Goli la full-back Bryan Oviedo lilimtosha kabisa Roberto Martinez kufanya kile Moyes alishindwa kukifanya katika miaka yake 11 ya kuwa boss wa Toffes – Kushinda ugenini katika dimba la United.


41: Mkwaju wa Yohan Cabaye mpaka kipindi cha pili ilihakikisha Newcastle ushindi wa 1-0 dimbani Old Trafford,hi indo kusema Magpies walirudi Tyneside na pointi zote tatu muhimu.Hii ni mara yao ya kwanza kabisa kushinda hivyo kwa takribani miaka 41


1978: Laurie Cunningham and Cyrille Regis were among the goals when West Bromwich Albion last won at Old Trafford back in 1978. This time around, Morgan Amalfitano and Saido Berahino were the heroes as the Baggies ended a 35-year wait for a win. West Brom had also failed to beat United in 13 prior attempts.


1978: Magoli ya Laurie Cunningham na Cyrille Regis yalikuwa ni miongoni ya magoli wakati West Bromwich Albion iliposhinda kwa mara ya mwishomwaka 1978. Sasa hivi Morgan Amalfitano and Saido Berahino wameibuka vidume baada ya Baggies kumaliza ukame wa miaka 35 ya kusubiri ushindi. West Brom nao wameshindwa kuifunga United kwa mara 13 walizokutana huko nyuma.


8: Southampton nao wamemaliza kimeo cha kufungwa na Man U mechi nane mfululizo shukrani kwa Adam Lallana kwa goli lake la kusawazisha la dakika za lala salama mwezi Oktoba.


26: Baada ya mechi zao 21 za premier League, United wameshapoteza point 29. Msimu uliopita walipoteza point 25 tu msimu mzima.


25:Namba ya asilimia ya mechi walizopoteza United mpaka sasa kwa msimu huu katika mashindano yote – 8 kwa 32. Wakati wa msimu uliopita, vidume wa Ferguson walipoteza 10 ya 54.

No comments:

Post a Comment