Pages

Tuesday, February 4, 2014

MTIBWA SUGAR, SIMBA KUUMANA MOROGORO LEO

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaingia raundi ya 16 Februari 5 mwaka huu kwa mechi tano huku Mtibwa Sugar ikiikaribisha Simba kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Kiingilio katika mechi hiyo ambayo itakuwa ya kwanza kuchezwa kwenye uwanja huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 10,000 tangu uanze mzunguko wa pili wa VPL kitakuwa sh. 5,000. Jonisia Rukyaa kutoka Bukoba ndiye atakayechezesha mechi hiyo.

Mechi nyingine za ligi hiyo ni Tanzania Prisons vs Coastal Union (Sokoine, Mbeya), Mgambo Shooting vs Ruvu Shooting (Mkwakwani, Tanga), Rhino Rangers vs Oljoro JKT (Ali Hassan Mwinyi, Tabora) na JKT Ruvu vs Ashanti United (Chamazi, Dar es Salaam).

No comments:

Post a Comment