Pages

Saturday, February 1, 2014

REAL MADRID KUUFANYIA MATENGENEZO UWANJA WA SANTIAGO BERNABEU - KUINGIZA WATU 90,000 UKIKAMILIKA


Raisi wa Real Madrid Florentino Perez jana alionyesha rasmi ramani mpya ya uwanja wa Santiago Bernabeu utakavyokuwa baada ya kufanyiwa marekebisho. Uwanja huo ambao ni mmoja wa miongoni mwa viwanja bora duniani unatarajiwa kuanza matengenezo hivi karibuni na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa 2017.

Perez amesema matengenezo hayo yatakuwa yakisitishwa kila wakati ambapo timu itakuwa ina mchezo wa nyumbani, kwa maana hiyo Madrid wataendelea kuutumia Santiago Bernebeu katika kipindi chote hiki cha matengenezo.


No comments:

Post a Comment