Pages

Saturday, February 8, 2014

PRISONS, RUVU SHOOTING KUUMANA SOKOINE LEO, SIMBA KESHO MKWAKWANI TANGA



Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea leo kwa mechi moja kati ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting itakayofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.



Mechi nyingine nne za ligi hiyo zitachezwa kesho Februari 9 mwaka huu kwenye viwanja mbalimbali. Mgambo Shooting vs Simba (Mkwakwani, Tanga), Oljoro JKT vs Kagera Sugar (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha), Rhino Rangers vs Coastal Union (Ali Hassan Mwinyi, Tabora) na Mbeya City vs Mtibwa Sugar (Sokoine, Mbeya).

No comments:

Post a Comment