Pages

Saturday, February 8, 2014

FDL YAANZA VUMBI LA MZUNGUKO WA PILI

Mzunguko wa pili wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) unaanza leo kwa mechi za kundi A na B wakati kundi C lenyewe litaanza mechi zake Februari 22 mwaka huu.



Mechi za kundi A ni Green Warriors vs Tessema (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi), Polisi Dar es Salaam vs Transit Camp (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam). Februari 9 mwaka huu ni African Lyon vs Villa Squad (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi) na Friends Rangers vs Ndanda (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam).



Kundi B kwa kesho (Februari 8 mwaka huu) ni Polisi Morogoro vs Burkina Faso (Jamhuri, Morogoro), Lipuli vs Mkamba Rangers (Samora, Iringa), Kurugenzi vs Kimondo (Wambi, Mufindi) na Mlale JKT vs Majimaji (Majimaji, Songea).

No comments:

Post a Comment