Pages

Monday, February 3, 2014

MAPACHA WATATU NA ACUDO KUKAMUA JUKWAA MOJA SIKU YA WAPENDANAO








BENDI za Mapacha watatu na Acudo Impact watafanya onyesho la pamoja kwenye sherehe za Siku ya wapendao katika Ukumbi wa Letas Lounge (Business Park), jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo la siku ya wapendanao ambalo hufanyika kila Februari 14 ya kila mwaka limepewa jina la “No biff Tupendane” litahusisha bendi mbili ili kuhakikisha wanatoa burudani ya uhakika kwa mashabiki wao siku hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini, Meneja wa bendi ya Mapacha watatu, Khamis Dacota alisema kuwa pia siku hiyo kila bendi itatambulisha wanamuziki wapya waliojiunga na bendi hizo.

“Lengo la bendi hizi kupanda jukwaa moja ni kufuta ile dhana iliyopo kwa wadau kuwa wasanii wa bendi hizi wana ugomvi sambamba na kutambulisha wasanii ambao wamejiunga kuongeza nguvu katika vikosi hivi”, alisema Dacota.

Pia alisema wataimba wimbo maalum kwa ajili ya siku hiyo wimbo ambao utaimbwa na bendi zote mbili kwani wameutunga kwa pamoja na wameufanyia mazoezi pamoja.
Vilevile watatoa zawadi maalum kwa wale wapendanao watakao kuwa wamependeza.

No comments:

Post a Comment