Pages

Monday, February 3, 2014

JUAN MATA ATETEA MAN U KWA KIPIGO KUTOKA KWA STOKE CITY, ASEMA WATAIRUDISHA TIMU KWENYE CHATI


Mchezaji mpya wa Mabingwa Manchester United, Juan Mata, amedai bahati mbaya iliyowasakama itaisha hivi karibuni.
Juzi Man United walikikwaa kipigo cha 8 kwenye Ligi Kuu England walipofungwa 2-1 na Stoke City huku Robin van Persie, Wayne Rooney na Mata wakianza Mechi ya kwanza pamoja kwa mara ya kwanza.
Lakini Mata anaamini bahati mbaya itaisha na amesema: “Bahati mbaya hatukushinda Mechi yetu ya pili wiki hiyo. Ni Uwanja mgumu na upepo mkali haukusaidia kucheza Soka. Lakini hatukustahili kufungwa!” 
Aliongeza: “Tulikuwa na bahati mbaya kwa Goli lao la kwanza, tukarudisha na tulijua tutashinda lakini tukafungwa la pili kwa Bao la bahati pia.All smiles: Charlie Adam (left) celebrates scoring in Stoke's 2-1 victory over the Red Devils on Saturday Tulipata nafasi nzuri hatukuzitumia. Lakini tunahisi hatuwezi kufungwa tena Gemu kama hizi. Natumai ile bahati iliyotoweka kwetu itarudi tena kwani tuna bahati mbaya hata kwenye Majeruhi. Tulipoteza Masentahafu wawili kabla Haftaimu. Lakini naamini tutaanza mbio za ushindi na kuwa bora zaidi!”Juan Mata

No comments:

Post a Comment