Pages

Sunday, February 9, 2014

MANCHESTER UNITED WABANWA MBAVU NA FULHAM WATOKA SARE WAKIWA NYUMBANI KWAO OLD TRAFFORD

Kocha wa Man United David Moyes akisalimiana na Rene Meulensteen wa Fulham
Manchester United, licha ya kutawala Mechi yote, kukosa Nafasi nyingi mno na hata kuweza kutoka nyuma kwa Bao 1-0 na kumudu kuongoza kwa Bao 2-1 walikatwa maini katika Dakika ya 94 wakati Darren Bent aliposawazisha kwa Bao laini.
Kipindi cha Pili, Man United walifanya mabadiliko kadhaa kwa kuwaingiza kina Valencia, Januzaj na Chicharito na hii ilileta uhai na waliweza kufunga Bao 2 katika Sekunde 90.


Lakini kosa kosa zao za kufunga Bao la 3 kuliwagharimu kwani bila kutarajiwa Bent aliisawzishia Fulham kwenye Dakika za Majeruhi na kupata Sare ya Bao 2-2.Michael Carrick akijiuliza kwa kile kilichotokea...Nemanja Vidic kwenye patashika na Muamer TankovicMchezaji wa Manchester United Robin van Persiekwenye patashika na mchezaji wa Fulham Sascha Riether ndani ya eneo hatari la lango la Fulham.Steve Sidwell akimmaliza kipa wa United David De Gea.Steve Sidwell akishangilia bao lake
Bao la Fulham limefungwa na Steve Sidwell katika dakika ya 19. Bao hilo limedumu mpaka dakika mwisho kwenye kipindi cha kwanza na timu ya Fulham ndio imekwenda mapumziko kwa bao 1-0 dhidi ya Wenyeji Man United kwenye uwanja wa Old Trafford.Kipindi cha pili dakika ya 78 Van Persie akasawazisha bao na kufanya 1-1, Dakika moja baadae United wakapata bao jingine la pili na kufanya 2-0 dhidi ya Fulham wanaoshikilia nafasi ya mwishoni mwa ligi hiyo pendwa ya EPL mwamuzi wa mtanange huo akiwa K. Friend‎.Mashabiki wa UnitedWayne roone akiwachambua wachezaji wa FulhamBao likifungwa na Michael Carrick katika dakika ya Dakika ya 80.
Ndani ya dakika za nyongeza Fulham wakapata bao na kusawazisha kwa kufanya 2-2. Mfungaji wa bao hilo akiwa ni Darren Bent katika dakika ya nyongeza.
Manchester United, licha ya kutawala Mechi yote, kukosa Nafasi nyingi mno na hata kuweza kutoka nyuma kwa Bao 1-0 na kumudu kuongoza kwa Bao 2-1 walikatwa maini katika Dakika ya 94 wakati Darren Bent aliposawazisha kwa Bao laini. Mechi inayofuata kwa Man United ni hapo Jumatano huko Emirates watakapoivaa Arsenal ambayo Jana ilikung’utwa Bao 5-1 na Liverpool huko Anfield.Rooney Chupuchupu afunge bao la tatuLast gasp: Manchester United were less than a minute from victory when Darren Bent headed home to snatch a point for FulhamDarren Bent aliposawazisha kwa Bao katika dakika za lala salama.Flying: Bent celebrates his dramatic equaliser at Old TraffordBent akishangilia bao lake la kusawazisha katika dakika ya majeruhiMajanga kwa Man United!!!

Kipa wa United hoi!! baada ya kusawazisha Fulham katika dakika za majeruhi..

No comments:

Post a Comment