Pages

Friday, February 28, 2014

EUROPA LEAGUE: NAPOLI 3 v SWANSEA CITY 1, RAFAEL BENITEZ AIONGOZA TIMU YAKE KUITUPA NJE SWANSEA

EUROPA LIGI Usiku huu ilikamilisha Mechi zake za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 32 na Vigogo, Juventus, Valencia, Sevilla na Fiorentina kusonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 lakini wengine, wakiwemo, Lazio na Ajax kutupwa nje.
NAPOLI 3 v SWANSEA CITY 1
Napoli imeipiga Swansea City Bao 3-1 na kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya EUROPA LIGI.
Timu hizi zilitoka Sare ya Bao 0-0 katika Mechi ya kwanza huko Wales.
Bao za Napoli zilifungwa na Insine, Higuaian na Inler huku Bao la Swansea likifungwa na Guzman.

Garry Monk akiwa hana raha kabisa baada ya kutupwa nje!!
Gonzalo Higuain akishangilia bao lake kwa timu yake Napoli kwa kufanya 2-1 mbele ya Swansea
Wachezaji wa Napoli wakipongezana baada ya kushinda

Mapema kocha wote wawili walisalimiana:Rafael Benitez (kulia) wa Napoli na Kocha wa Swansea Garry Monk.

Gokhan Inler akifunga bao la tatu na kufanya 3-1 na kuipa ushindi Napoli kwenye muda wa mwishoni wa dakika za lala salama..

Kipa wa Swansea Vorm akisungukwa na mchezaji wa Napoli fowadi Marek Hamsik

No comments:

Post a Comment