Pages

Friday, February 28, 2014

AL AHLY YAIHOFIA YANGA






KOCHA Mkuu wa Al Ahly ya Misri, Mohammed Youssef, amesema watacheza kwa tahadhari kumhofia Mrisho Ngassa kwenye mchezo wa Jumamosi.

Al-Ahly ambayo inaaanza kampeni ya kutetea ubingwa wake kwa vilabu bingwa barani Afrika, itakapomenyana na mabingwa wa Tanzania, Young Africans,maarufu kama YANGA, jijini Dar es Salaam, mchezo utakaochezwa Uwanja wa Taifa.

Youssef aliyasema hayo jana walipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, (JNA) Dar es Salaam.
“Tumekuja kushindana na naamini tutafanya vizuri lakini tutacheza kwa umakini kutokana na safu ya ushambuliaji ya Yanga kuwa nzuri hasa Mrisho Ngassa kwani ana mbio na uwezo wa kufunga mabao”, alisema Youssef.

Al Ahly iliwasili jana alfajiri saa 12 kasorobo kwa Shirika la Ndege la Misri Egypt Air kikiwa na watu 35 wakiwemo wachezaji 22, bechi la Ufundi 8 pamoja na viongozi 5 na wamefikia katika Hotel ya Hyatt Kempsinki ambapo ndio itakuwa ikiweka kambi.

Siku ya Jumatano na Alhamisi  jioni watafanya mazoezi katika Uwanja wa IST uliopo Upanga, na Ijumaa jioni watapata fursa ya kufanya mazoezi katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam tayari kwa mchezo huo wa Jumamosi.

Tiketi za mchezo huo zinaanza kuuzwa leo kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam na kiingilio cha juu ni  Shs 35,000,  25,000,  13,000 na cha chini kwa viti vya kijani na bluu ni Sh. 7000.

Rekodi ya Al Ahly:
Wana mataji 19 moja zaidi ya mataji 18 ya Ac Milan ya Italia
Al Ahly imeshinda mara 8 kombe la mabingwa barani Afrika, mwaka 1982, 1987,2001,2005,2006, 2008, 2012, na 2013.

Makombe 4 ni ubingwa wa Kombe la washindi 1984, 1985, 1986, 1993.
Mara sita imetwaa kombe la CAF Super Cup 2002, 2006, 2007, 2009, 2013, na 2014 na mmoja likiwa la Afro-Asian Cup mwaka 1988.

Rekodi ya Yanga
Yanga ilishawahi kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1998

No comments:

Post a Comment