Pages

Tuesday, January 28, 2014

VPL KUTIMUA VUMBI TANGA, BUKOBA, DAR


Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kesho kwa Coastal Union kuikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini.

Kiingilio katika mechi hiyo ni sh. 5,000 na sh. 15,000. Nayo Ruvu Shooting na Mbeya City zitapambana kwenye Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani kwa viingilio vya sh. 10,000 na sh. 5,000.

Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Kagera Sugar na Mtibwa Sugar. Viingilio ni sh. 5,000 na sh. 3,000.

Azam itaumana na Rhino Rangers katika Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Mbagala. Viingilio ni sh. 10,000 na sh. 3,000.

No comments:

Post a Comment