Pages

Monday, January 27, 2014

SIMBA YAICHAPA RHINO UWANJA WA TAIFA









SIMBA SC imeanza vyema mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hadi mapumziko, tayari Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililotiwa kimiani na mshambuliaji Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’ dakika ya 14.
 Ushindi huo, unaifanya Simba SC itimize pointi 28 baada ya kucheza mechi 14, ikibaki nafasi ya nne nyuma ya Yanga yenye pointi 31, Azam na Mbeya City pointi 30 kila moja. 
Messi alifunga bao hilo, baada ya kutokea mpira wa piga nikupige langoni mwa Rhino na ndipo akaupitia mpira na kufumua shuti kali lililoipa ushindi huo Simba SC.
Pamoja na kufungwa, Rhino walicheza vizuri na kuonyesha upinzani kwa Simba SC ambao katika mechi ya mzunguko wa kwanza walitoka nayo sare ya 2-2 Uwanja wa Ally Hassan Mwinyhi Tabora.  

No comments:

Post a Comment