Pages

Saturday, January 25, 2014

RAIS WA BARCELONA ROSELL AJIUZULU KWA TUHUMA ZA UBADHIRIFU WA UHAMISHO WA NEYMAR

 

Rais wa Barcelona Sandro Rosell amejiuzulu na Barcelona imetinga Mahakamani wakichunguzwa kwa Ubadhirifu wa Fedha kwenye Uhamisho wa Supastaa wa Brazil Neymar kutoka Santos kwenda Barca mwanzoni mwa Msimu.

Sandro Rosell amejiuzulu urais wa Barcelona

Sandro Rosell

Josep Maria Bartomeu
Barca wanadaiwa kumnunua Neymar kwa Dau la Euro Milioni 57.1 lakini ni Euro Milioni 17.1 tu ndizo zilifika mikononi mwa Klabu yake Santos ya Brazil huku nyingne zote zikikombwa na Wamiliki wengine waliokuwa na haki nae.
Lakini baadhi ya Wamiliki hao wameibuka na kudai hawakupata mgao wowote wakiwemo Wamiliki wa Maduka Makubwa, DIS, huku Kampuni ya N&N, inayomilikiwa na Baba yake Neymar ikisemekana imekomba Euro Milioni 40.
Hivi sasa, Kesi ipo Mahakamani kwenye hatua za awali za uchunguzi, na itasikilizwa na Jaji Pablo Ruz, ambae anatarajiwa kukusanya taarifa toka kwa Neymar, Santos na Barcelona kabla hajamwita Rosell aende mwenyewe Mahakamani kutoa Ushahidi.

Kesi hii inafuatia malamiko ya Mwanachama wa Barcelona, Jordi Cases, ambae ameungwa mkono na Waendesha Mashitaka wa Spain waliokubaliana na Madai yake kwamba kulikuwepo ubadhirifu na ukiukwaji wa Sheria kwa kutumia Mkataba Feki.


Sandro Rosell (kushoto) na Neymar (kulia) walipomsajili hivi karibuni

Jordi Cases, Mwanachama wa Barcelona, alifungua Kesi Mahakamani akidai Ubadhirifu wa Fedha na kutokuwepo uwazi kwenye Uhamisho wa Neymar.
Cases amedai asingefungua Kesi hiyo kama uongozi wa Barca ungemjibu kistaarabu alipohoji undani wa Uhamisho wa Neymar.
Barcelona, Neymar na Kampuni ya N&N ilisaini Mkataba Mjini Sao Paulo, Brazil Mwaka 2011 wa Neymar kuhamia Barcelona Mwaka 2014.

Mkataba huo uliposainiwa, upande wa Neymar ulipokea Malipo ya Euro Milioni 10 kama Mkopo ambao ungelipwa baada Neymar kuhamia Barca.
Pia uliweka Dau la Euro Milioni 40 kama haki za Neymar na pia Adhabu ya Euro Milioni 40 ikiwa Makataba huu utakiukwa.

Lakini Mwaka Jana, Santos na Barca, zilikubaliana Neymar ahame Mwaka mmoja kabla ya makubaliano ya awali na hivyo Barca kulazimika kulipa Adhabu ya Euro Milioni 40 ikiwa Makataba huu utakiukwa.
Hilo ndio limeibua wasiwasi kwenye Mamlaka za Spain baada Shabiki Jordi Cases kulalamika.
Rosell anatuhumiwa ubadhirifu wa Fedha ambao huko Spain Adhabu yake ni Kifungo kuanzia Mwaka mmoja hadi nane.

No comments:

Post a Comment