Pages

Saturday, January 25, 2014

MBEYA CITY NA AZAM FC ZAENDELEA KUIFUKUZIA YANGA KILELENI BAADA YA KUSHINDA MICHEZO YAO LEO




TIMU ya Azam FC na Mbeya City zimeendelea kuifukuzia Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya zote kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Azam iliifunga Mtibwa Sugar uwanja wa Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, huku Mbeya City ikiichapa Kagare Sugar mjini Bukoba.

Ushindi huo umezifanya Azam na Mbeya City zote kufikisha pointi 30, moja nyuma ya Yanga yenye pointi 31 baada ya kushuka dimbani mara 14.
Katika mchezo wa Azam na Mtibwa, timu zote zilianza kwa kushambuliana kwa zamu, huku Azam ikionekana kulisakama lango la Mtibwa kwa kasi zaidi, lakini uimara wa mabeki wake waliweza kukoa hatari kadhaa.

Pasi iliyopigwa na Joseph Kimwaga iliweza kumpata vizuri, Tchetche aliyefunga bao hilo pekee baada ya kuweza kuwachomoka mabeki wa Mtibwa na kufumua shuti lililojaa moja kwa moja wavuni.

Kikosi cha Azam kilikuwa; Mwadini Ali, Malika Ndeule, Erasto Nyoni, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Brian Umony/Ismael Kone dk13/Khamis Mcha dk71, Kipre Tchetche na Joseph Kimwaga/Seif Karihe dk69.

Mtibwa Sugar; Hussein Sharrif, Hassan Ramadhani, Said Mkopi, Salim Mbonde, Salvatory Ntebe, Shaaban Nditi, Shaaban Kisiga, Masoud Ally/Abdallah Juma dk62, Juma Luizio/Mussa Mgosi dk84, Jamal Mnyate na Vincent Barnabas/Mohamed Salum dk75.

Katika mchezo mwingine, Coastal Union ilitoka sare ya kufungana bao 1-1, JKT Oljoro mchezo uliopigwa uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

No comments:

Post a Comment