Bingwa wa michezo ya all African Games mwaka 1973 ndg Kipchoge Keino (KULIA) wa Kenya ambaye ndiye mkimbizaji wa kifimbo cha malkia akiwa na mmliki wa blog ya Lenzi ya michezo |
Watoto wa shule ya Filbert Bayi wakicheza ngoma |
JKT Mgulani |
MJUMBE wa Baraza la
Michezo ya Jumuiya ya Madola, Kipchoge
Keino ameitaka serikali kuweka mipango dhabiti ya kuendeleza michezo.
Keino ambaye ndiye mkimbizaji wa kifimbo cha malkia
aliyasema hayo wakati alipotua Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere na kupokele na viongozi wa
serikali na kamati ya Olmpiki Tanzania.
“Tanzania ina vipaji na hili nalijua kwani nilikuwa na
Filbert Bayi kwenye mashindano mbalimbali ya kimataifa hivyo mikakati ikiwekwa
ya kuendeleza vipaji nchini itapata medali nyingi kwenye mashindano ya
kimatifa”’ alisema Keino ambaye alishawahi kuwa bingwa wa mashindano ya Afrika
(all African Games)
Kifimbo hicho kiliktua nchini kikitokea nchini Rwanda na
kukabidhiwa kwa Rais wa Kamati ya
Olympiki Tanzania Rashid Gulam na leo kitakimbizwa katika mitaa na barabara
kadhaa za jijini la Dar es Salaam na Baadae kitapelekwa Ikulu kabla ya kwenda
Zanzibar .
“Kifimbo cha Malkia kesho kitakuwa hospitali
ya Muhimbili kwenye wodi ya watoto wenye ugonjwa wa saratani ili wacheze
nacho, baadae kitapelekwa Uwanja wa
Taifa ili watu wakione na kupiga picha, baadae kitakimbizwa katika barabara ya
Nelson Mandela kikifika TAZARA kitapitia barabara ya Nyerere kurudi mjini
kupitia Gerezani baadae kitapelekwa
Ikulu ambako kitapokelewa na Rais Jakaya Kikwete:, alisema Jabir ambaye ni katibu wa kamati Maalum ya
TOC”, alisema
“Kikiwa Zanzibar kitakimbizwa Mji Mkongwe na sehemu nyingine
za Historian a baadae kitapelekwa Ikulu ya Zanzibar”, alisema
Pia Jabir aliwataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam
kujitokeza kwa wingi kukimbiza kifimbo hicho kwani watanzania wana historia ya
kuwa wakarimu.
No comments:
Post a Comment