Pages

Saturday, December 7, 2013

YANGA YAIIENDEA SIMBA BEACH KWA AJILI YA NANI MTANI JEMBE


Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezini leo asubuhi katika fukwe za Coco


Kikosi cha Mabingwa wa Ligi Kuu ya soka Tanzania bara Young Africans leo wameendelea na mazoezi  kwa kujifua katika fukwe za Coco kujiandaa na mchezo wa Hisani "Nani Mtani Jembe" dhidi ya Simba SC Disemba 21, 2013 katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kikosi cha mholanzi Ernie Brandts baada ya kufanya mazoezi ya uwanjani kwa kipindi cha takribani wiki mbili, leo kilikuwa kikijifua katika fukwe za Coco ambapo mazoezi ya stamina, na viungo ndio yalitwala zaidi.
Mara baada ya mazoezi ya leo kocha Brandts anasema anashukuru programu yake inakwenda vizuri, wachezaji wote wanaendelea na mazoezi na hakuna majeruhi hata mmoja tangu waanze maandilizi ya mzunguko wa pili hivyo anaamini kikosi chake kinaendelea kuimarika zaidi.
"Ukiwa na wachezaji wako wote wapo fit ni jambo jema, kwani unapata fursa ya kutoa maelekezo kwa wakati mmoja, kuwatambua na kuwasimamia jinsi wanavyoyashika na kuyatumia katika kujenga timu bora" alisema Brandts
Young Africans imekua ikiendelea na mazoezi kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya klabu Bingwa Afrika ambayo inatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi wa Februari 2014.

Timu itaendelea kufanya mazoezi kila siku kulingana na programu ya mwalimu mpaka wachezaji wengine waliopo na vikosi vya timu za Taifa katika mashindano ya CECAFA Challenge nchini Kenya watakaporejea na kujumuika na wenzao katika maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo wa "Nani Mtani Jembe" .

No comments:

Post a Comment