Pages

Saturday, December 21, 2013

SIMBA YAIADHIBU YANGA TAIFA LEO KWA KUIFUNGA 3-1 MECHI YA MTANI JEMBE



 



 

TIMU ya Simba leo imeifunga Yanga mabao 3-1 kwenye mchezo wa nani mtani jembe na kuondoka na kitita cha milioni 100, medali za dhahabu na kombe.

Simba ambayo haikupewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo kabla ilianza kuandika bao la kwanza kupitia kwa Amis Tambwe aliyefunga mawili huku Juma Awadh akipigilia msumari wa mwisho.

Katika mchezo huo Simba ilianza kuhesabu bao lake la kwanza katika dakika ya 13 lilofungwa na Tambwe baada ya kazi nzuri ya Ndemla.

Wakati Yanga ikijaribu kutaka kusawazisha bao hilo, Simba ilifunga bao la pili kwa mkwaju wa penalti dakika ya 42 iliyofungwa na Tambwe baada ya David Luhende kumuangusha Ramadhani Singano eneo la hatari.

Katika kipindi cha pili, uzembe wa golikipa mpya wa Yanga, Juma ulimuwezesha Awadh Juma kuifungua kirahisi Simba bao la tatu.

Yanga ilipata bao lake la kufutia machozi kupitia kwa mchezaji aliyesajiliwa hivi karibuni, Emmanuel Okwi aliyefunga kwa kichwa dakika ya 89 akiunganisha krosi ya Haruna Niyonzima.

Timu zote zilifanya mabadiliko ya wachezaji katika kipindi cha pili, ambapo Simba iliwatoa, Henry Joseph, Ndemla, Chanongo, Awadh na Ramadhani Redondo, huku nafasi zao zikichukuliwa na Singano, Seleman Uhuru, Zahoro Pazi na Humud.

Huku Yanga ikiwatoa, Athuman Idd ‘Chuji’, Hamisi Kiiza, Didier Kavumbagu, Haroub Cannavaro na Mrisho Ngassa, huku nafasi zao zikichukuliwa na Emmanuel Okwi, Simon Mvusa, Dilunga,Juma Abdul na Jerryson Tegete.
Katika mchezo huo, Yanga ilimpoteza Kelvin Yondani aliyooneshwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya, Singano.

No comments:

Post a Comment