Pages

Tuesday, December 31, 2013

NICOLAS ANELKA KUKUMBANA NA ADHABU ZA FA, BAADA YA KUSHANGILIA GOLI JUZI KWA ALAMA ILIYOONEKANA NI YA KIBAGUZI

Nicolaus Anelka huenda akakumbana na Kifungo Mechi 5 na kuendelea kwa kushangilia Goli Timu yake, West Bromwich Albion, ilitpotoka Sare 3-3 na West Ham Jana Jumamosi, kwa kutumia ishara ya Saluti ambayo inahusishwa na Mafashisti wa Nazi
Saluti hiyo [Pichani] juu ambayo Mkono wake wa kushoto aliupitisha Kifuani na Mkono wa Kulia kuelekezwa chini huchukuliwa kama Saluti ya Nazi kwa kinyume lakini mwenyewe Anelka amekiri hiyo inaitwa ‘Quenelle’ ili kumsapoti Rafiki yake wa France, Dieudonné M'Bala M'Bala, ambae ni Mchekeshaji, anaesakamwa Nchini humo kwa kuwa Mbaguzi.
Saluti hiyo ya Anelka imezua kizaazaa kikubwa huko Ufaransa kiasi ambacho Waziri wa Michezo Nchini humo, Valérie Fourneyron, amesema inatia kinyaa.
Huko England, FA, Chama cha Soka England, na Kick It Out, Taasisi inayopambana na Ubaguzi, wote wamesema wanafanya uchunguzi.

Anelka alitumia hiyo ‘Quenelle’ akisheherekea Bao lake la Kwanza kati ya mawili iliyofunga kwenye Sare hiyo ya 3-3 kati ya Timu yake West Brom na West Ham na hilo likiwa Bao lake la Kwanza kwa Klabu hiyo tangu ajiunge nayo mwanzoni mwa Msimu.
Klabu ya West Brom imeibuka na kumsapoti Anelka ambae Mwaka 2004 alisilimu na kuwa Muislam.

Lakini Anelka si Mwanasoka wa kwanza kupigwa Picha akitoa hiyo ‘Quenelle’ kwani Samir Nasri wa Manchester City na Mamadou Sakho wa Liverpool walishanaswa wakiwa pamoja na Dieudonné wakitoa Saluti hiyo ingawa Sakho baadae alisisitiza hakujua maana yake na alihadaiwa kuitumia.


Defiant: A group performs the 'quenelle' salutes in front of the theatre Dieudonne's performing at

Friends: West Brom acting head coach Keith Downing says that the gesture was a dedication from Anelka (right) to his French comedian friend Dieudonne (left), which Anelka reiterated on Twitter

No comments:

Post a Comment