Mechi
ya Nani Mtani Jembe kati ya Yanga na Simba iliyochezwa juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi
wa mabao 3-1 imeingiza sh. 422,611,000.
Mapato
hayo ni kutokana na washabiki 52,589 waliokata tiketi kushuhudia mechi
hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh.
20,000 na sh. 40,000. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia
watazamaji wengi ambapo walikuwa 19,044.
Asilimia
18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato
hayo ni sh. 64,466,084.75 wakati gharama za kuchapa tiketi ni sh.
7,488,000.
Mgawo
mwingine ilikuwa kama ifuatavyo; kila klabu imepata sh. 117,470,066.61,
asilimia 15 ya uwanja ni sh. 52,598,537.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira
wa Miguu (FDF) sh. 35,065,691.53 wakati gharama za mchezo zilikuwa sh.
28,052,553.22.
No comments:
Post a Comment