Pages

Thursday, December 19, 2013

MAJANGA LIGI KUU ENGLAND!! VAN PERSIE, WAYNE ROONEY, ANDROS TOWNSEND, SERRGIO AGUERO NJE


Mchezaji Andros Townsend wa Tottenham aliumia walipokuwa wanacheza na West Ham kwenye ligi ya Capital One Cup.

Townsend kuumia kwake uwanjani White Hart Lane wenda akarudi uwanjani baada ya mwaka mpya.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Manchester City, Sergio Aguero kuna uwezekano wa kukosa mchezo Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona baada ya kuumia msuli wa kigimbi. Meneja wa City Manuel Pellegrini alithibitisha kuumia kwa nyota huyo katika mchezo ambao timu yake ilishinda kwa mabao 6-3 dhidi ya Arsenal Jumamosi iliyopita ambapo alidai kuwa naweza kukosekana uwanjani kwa kipindi cha miezi nane. Pellegrini amesema kwa mujibu wa madaktari Aguero anaweza kukaa nje kwa muda wa mwezi mmoja au inaweza kuwa wiki nane. Kama nyota huyo akikaa nje kwa wiki nane atakosa mechi 12 ikiwemo na mchezo dhidi ya Barcelona utakaochezwa Februari 18 mwakani.
Sergio Aguero
Van Persie yeye yupo nje kujiuguza Nyama za Paja na wenda akazikosa mechi 8 au ziadi, aliumia kwenye mtanange na dhidi ya Shakhtar Donetsk jumanne iliyopita kwenye Champions League baada ya kupiga kona iliyozalisha bao kwa United lililofungwa na Phil Jones.Wayne Rooney jana hakucheza kwenye Capital One Cup walipokuwa wanacheza na Stoke City baada ya kuthibitishwa na kocha wake David Moyes kuwa kaumia na wenda akarudi kilingeni baada ya sikukuu za mwaka mpya. Hivyo anahitaji kupumzishwa kwa muda..

No comments:

Post a Comment