Pages

Saturday, December 28, 2013

KOCHA WA CARDIFF MALKY MACKAY KIBARUA AFUKUZWA, KOCHA WA KUZIBA NAFASI YAKE KUTEULIWA HIVI KARIBUNI

Malky Mackay
Sakata kuhusu hatma ya kocha Malky Mackay katika klabu ya Cardiff, imefika kikomo baada ya klabu hiyo kuthibitisha kuwa amefutwa kazi.
Kufutwa kwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 42, kulikuwa kumebashiriwa, baada ya mmiliki wa klabu hiyo Vincent Tan, kumtumia barua pepe wiki iliyopita kumtaka ajiuzulu au afutwe kazi. 

Hata hivyo, onyo hilo lilifutiliwa mbali baada ya mwenyekiti wa klabu hiyo Mehmet Dalman kutangaza kuwa kocha huyo atasalia, kwa muda usiojulikana, lakini baada ya Cardiff kunyukwa magoli matatu kwa bila na Southampton
siku ya Alhamisi, mechi hiyo imegeuka na kuwa ya mwishi kwa kocha huyo wa zamani wa Watford.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na wasimizi wa klabu hiyo siku ya Ijumaa, kocha huyo sasa amefutwa kazi rasmi.
Taarifa hiyo imesema kuwa kocha mpya atateuliwa hivi karibuni.
Kocha Mackay alitokea Watford kuja Cardiff mwezi wa sita 2011Siku za raha alizokuwa nazo wakati anateuliwaKupanda kwake Ligi kulitegemea nguvu na mbinu za kocha huyo kuwaongoza vizuri CardiffKocha Malky Mackay uwanjani
Pamoja na kufukuzwa Cardiff Kocha huyo aliiongoza na kushinda mechi kumi za nyumbani kubadilika na kujikuta wako juu kwenye Ligi kabla ya kupanda ligi kuu England mwaka jana.Hata muda mwingine wakitosha nguvu na timu pinzani walifurahia pia!!Kubebwa kwake ilikuwa ni furaha kwa wote, timu pamoja na viongozi Furaha za ushindi kwa timu ya Cardiff baada ya kuifunga Bolton kipindi cha nyuma.Mackay na mmiliki Vincent Tan wa CardiffKocha Malky aliiongoza Cardiff kuifunga Manchester City bao 3-2 kwenye msimu huu wa kwanza wa ligi kuuKocha hapa akitoa meno 32 yote

No comments:

Post a Comment