Pages

Saturday, December 28, 2013

ANDY MURRAY AREJEA KWA KISHINDO BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI WA MGONGO


Andy Murray ameandika ushindi wake wa kwanza tangu kurejea katika tenis baada ya kufanyiwa upasuaji wa mgongo.
Bingwa huyo wa michuano Wimbledon na mchezaji namba moja wa tenis kwa ubora nchini England amemshinda Stanislas Wawrinka kwa seti 6-3 6-4 katika michuanoa ya 'Mubadala World Tennis Championship' mjini Abu Dhabi.
Murray mwenye umri wa miaka 26 alipoteza kwa Lo-Wilfried Tsonga alhamisi katika mchezo wake wa kwanza tangu kurejea uwanjani baada ya upasuaji mwezi Septemba.
Amekaririwa akisema
"Ni vizuri kupata michezo miwili dhidi ya wachezaji wakubwa, ulikuwa ni mwanzo mzuri."
Murray anashikilia nafasi ya nne kwa ubora dunia atarejea katika tenisi ya ushindani katika michuano ya Exxon Mobil Open mjini Qatar wiki ijayo katika maandalizi yake ya kuelekea katika michuano mingine mikubwa ya Australian Open ambayo itaanza mjini Melbourne  Januari 13.
Mchezaji huyo bora wa tuzo ya mwaka ya BBC 2013 BBC Sports Personality ameongeza kwa kusema
"Najisikia vizuri zaidi ya nilivyokuwa miezi michache iliyopita, sasa nahitaji kucheza michezo mingi kama hii kwani itanipa mazoezi zaidi".

No comments:

Post a Comment