Leo
kwenye Dabi ya Jiji London Arsenal wakichezea kwenye uwanja wao
Emirates kuwakaribisha timu ya Chelsea wametoshana nguvu ya bila
kufungana huku timu zote zikiandamana pasipo kuliona lango la mwenzake,
Huku Arsenal ikiwania ushindi kurudi tena kileleni mwa Ligi Kuu England
wameshindwa kufunga na hatimaye kukwama kurudi kileleni kwa sare hiyo.
Timu zote zimejitahidi vya kutosha lakini ufundi wa kuweza kuifunga timu
nyingine ulikosa na umakini wa kuweza kukatiza mabeki ulikuwa finyu kwa
timu zote.Arsene Wenger na Jose Mourinho wakisalimiana hapa kwa kupeana mikono kweupe Emirates. Sare
hii inawabakisha Liverpool Kileleni wakiwa na pointi 36 na Arsenal
nafasi ya pili wakiwa na pointi 36 wakitofautina magoli ya kufunga.
Nafasi ya tatu ni Manchester City wenye pointi 35 wakifuatiwa na wenye
pointi 34 sawa na timu ya tano Everton wakitofautiana magoli.
Eden Hazard akitaka kumtoka Aaron RamseyLampard akipaisha mpira juu ya lango la Arsenal
Fernando Torresakiruka juu kuona kama ataziona nyavu za Arsenal
Gary Cahill na Olivier Giroud kwenye patashika..
Lampard na Mesut Ozil hawakupeana nafasi hii leo!!
Wachezaji wa Arsenal wakitofautina na wenzao Chelsea Emirates
...Kama kipa vile nasubiri mpira langoni!!!Torres chupuchupu afunge!
Mourinho akimpa msaada wa kumyanyua juu Sagna baada ya kupewa kigingi na Lampard
Frank Lampard na Bacary Sagna chini Kuna muda Joes Mourinho alipaki kimyaaaa akijiuliza kunani hapa Emirates!Theo walcott akionesha kiwangoWalcott akimfanyia ndivyo sivyo Cesar Azpilicueta... Torres nao na Per Mertesacker majanga chini.....Bora Sare kuliko kufungwa!! Lampard na John Terr wakiwasalimia mashabiki baada ya mpira kumalizika kwa sare!
Arsenal: Szczesny 6, Sagna 7, Mertesacker 7, Vermaelen 7, Gibbs 7, Ramsey 6, Arteta 7, Walcott 6, Ozil 6, Rosicky 6, Giroud 6.
Subs: Podolski, Monreal, Cazorla, Flamini, Fabianski, Bendtner, Jenkinson.
Chelsea: Cech 6, Ivanovic 7, Cahill 7, Terry 7, Azpilicueta 7, Mikel 6, Lampard 7, Ramires 6, Willian 6, Hazard 7, Torres 6.
Subs: Cole, Luiz, Mata, Oscar, Schurrle, Schwarzer, Eto'o.
Referee: Mike Dean
Subs: Podolski, Monreal, Cazorla, Flamini, Fabianski, Bendtner, Jenkinson.
Chelsea: Cech 6, Ivanovic 7, Cahill 7, Terry 7, Azpilicueta 7, Mikel 6, Lampard 7, Ramires 6, Willian 6, Hazard 7, Torres 6.
Subs: Cole, Luiz, Mata, Oscar, Schurrle, Schwarzer, Eto'o.
Referee: Mike Dean
MSIMAMO ULIVYOBAKIA BAADA YA KUMALIZA RAUNDI YA 17
Pos. | Logo &Team | P | W | D | L | GD | Pts |
---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | Liverpool | 17 | 11 | 3 | 3 | 23 | 36 |
2 | Arsenal | 17 | 11 | 3 | 3 | 16 | 36 |
3 | Manchester City | 17 | 11 | 2 | 4 | 31 | 35 |
4 | Chelsea | 17 | 10 | 4 | 3 | 14 | 34 |
5 | Everton | 17 | 9 | 7 | 1 | 13 | 34 |
6 | Newcastle United | 17 | 9 | 3 | 5 | 2 | 30 |
7 | Tottenham Hotspur | 17 | 9 | 3 | 5 | -5 | 30 |
8 | Manchester United | 17 | 8 | 4 | 5 | 8 | 28 |
9 | Southampton | 17 | 6 | 6 | 5 | 4 | 24 |
10 | Stoke City | 17 | 5 | 6 | 6 | -4 | 21 |
11 | Swansea City | 17 | 5 | 5 | 7 | 0 | 20 |
12 | Hull City | 17 | 5 | 5 | 7 | -6 | 20 |
13 | Aston Villa | 17 | 5 | 4 | 8 | -6 | 19 |
14 | Norwich City | 17 | 5 | 4 | 8 | -14 | 19 |
15 | Cardiff City | 17 | 4 | 5 | 8 | -12 | 17 |
16 | West Bromwich Albion | 17 | 3 | 7 | 7 | -5 | 16 |
17 | West Ham United | 17 | 3 | 5 | 9 | -8 | 14 |
18 | Crystal Palace | 17 | 4 | 1 | 12 | -16 | 13 |
19 | Fulham | 17 | 4 | 1 | 12 | -17 | 13 |
20 | Sunderland |
No comments:
Post a Comment