Pages

Friday, December 27, 2013

AZAM ILIPOIFUNGA RUVU SHOOTING 3-0 JANA CHAMAZI

TIMU ya Azam FC juzi iliwapa zawadi ya’boxing day’ mashabiki wake, baada yakuifunga Ruvu Shooting mabao 3-0 katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Azam wakiwa na kocha wao, Joseph Omog walikwenda mapumziko walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na  John Bocco, dakika ya 10 na bao la pili lilifungwa na Kipre Tchetche dakika ya 30 kwa penati baada ya Ayoub Kilata kushika mpira uliokuwa unaelekea golini.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko ambapo Azam walimwingiza mshambuliaji wao mpya Muamad Ismael Kone, raia wa Ivory Coast waliyemsajili katika dirisha dogo.

Kone alionyesha uwezo mkubwa wa kucheza soka na akafunga bao la tatu dakika ya 57.

Mchezo huo ulichezeshwa na mwamuzi Israel Nkongo ulikuwa maalum kwa Shirikisho la Soka kujaribu matumizi ya tiketi za elektroniki kabla haijaanza kuzitumia rasmi kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Akizungumza na baada ya mchezo huo Meneja wa timu hiyo, Jemadari Said alishukuru kwa ushindi walioupata na kusema kuwa timu ipo kwenye maandalizi ya kombe la mapinduzi ambao ndio mabingwa.

“Nashukuru tumeshinda mchezo huu kwani ni moja ya maandalizi ya kombe la Mapinduzi yanayotarajiwa kuanza Januari mosi, mwakani na sisi ndio mabingwa watetezi”, alisema Kazumari.
Kone alifunga bao moja katika ushindi huo
Kiungo Salum Abubakar 'Sure Boy' akimtoka mchezaji wa Ruvu 
Brian Umony akimiliki mpira mbele ya beki wa Ruvu
Beki David Mwantika akimtoka mchezaji wa Ruvu
John Bocco akipambana na wachezaji wa Ruvu
Kiungo wa Azam, Kipre Michael Balou akimdhibiti mchezaji wa Ruvu
Kocha mpya wa Azam, Joseph Marius Omog aliiongoza timu katika mechi ya kwanza leo
Gaudence Mwaikimba na beki wa Ruvu
Wapenzi wa Azam jukwaani
Waandishi maarufu wa habari za michezo, Mgaya Kingoba kulia na Amir Mhando kushoto walikuwepo Chamazi                                                                                                                                                                                                                                                                    





No comments:

Post a Comment