Pages

Thursday, November 7, 2013

YANGA YAMALIZA MZUNGUKO KWA KUICHAPA JKT OLJORO 3-0 NA KUKWEA KILELENI




YANGA imemaliza mzunguko wa kwanza wa ligi huku ikiwa inaongoza ligi hiyo kwa pointi 28 huku ikiziacha timu za Azam Fc pamoja na Mbeya City zikiwa zote na pointi 27.

Katika mchezo wa Uwanja wa Taifa Dar es salaam Yanga iliandika bao la kwanza kupitia mchezaji wake Simon Msuva katika dakika ya 25  ya mchezo baada ya kuaptiwa pasi safi na Haruna Niyozima.
Dakika ya 30 mshambiliaji wa Yanga, Mrisho Ngasa aliachia shuti kali akiwa katikati ya uwanja na kuandika bao la pili la timu hiyo.

Ngasa mnano dakika ya 53 alioneshwa kadi ya njano kufuatia kumchezea vibaya mchezaji Amir Omary.
Harakati za Ngasa za kuongeza bao jingine zilizaa matunda katika dakika ya 56 baada ya kutoa pasi safi iliyomkuta Jerryson Tegete ambae aliumalizia mpira huo uliomwacha kipa wa JKT Oljoro Damas Kugesha akiwa chini.

Yanga ilijitaidi kuendelea kutafuta magoli huku mchezaji wake Simon  Msuva akiwa anaendeleza harakati za kufunga lakini hata hivyo alipoteza pasi nyingi za mara kwa mara.
Kuna wakati Msuva alishindwa kumalizia pasi ya wazi aliyopewa na mchezaji Jerryson Tegete.
Mchezaji Niyozima alitolewa nje na kuingia Bahamuzi ambae nae iwapo angetumia vema kufunga magoli nafasi alizokuwa akizipata huenda Yanga ingemaliza mzunguko huo kwa 4-0.

Kuna wakati Bahamuzi alibakia na kipa wa JKT Oljoro lakini hata hivyo shuti lake lilitoka nje ya uwanja.
Amisi Kiiza nae iwapo asingekuwa mchoyo wa pasi basi huenda angeiwezesha Yanga kupata mabao mengi zaidi.
Uchoyo huo wa pasi ndio uliopelekea kocha wa Yanga Ernest Brandits kumgtoa nje na kisha kumuingiza Jerryson Tegete alieipatia Yanga bao la tatu.

Kutolewa kwa Kiiza na kuingizwa Tegete kulimchukiza mchezaji huyo hadi alifikia hatua ya kutoka kabisa nje ya benchi la ufundi na kwenda kukaa kwenye jukwaa la mashabiki wa Yanga.
Wakati mechi ilipoisha wakati wachezaji hao wakienda kwenye chumba cha kubadilishia nguo huku wakiwa na mazungumzo na Mwenyekiti wao Yusuph Manji, Kiiza alitoka nje ya chumba hicho huku akiwa amekasirika.

Kiiza alienda hadi nje ya uwanja ambapo alisikika akizungumza na baadhi ya wapenzi wa timu hiyo ambapo alikuwa akilalamikia hatua hiyo yakutolewa nje na kocha.
Kama haitoshi aliendelea kulalama na kufikia hatua ya kusisitiza kuwa kocha huyo alikuwa hampendi na ndio maana alimtoa huku akiwa bado ana hali ya mchezo.

" Mimi ni mchezjai na mwenye uwezo lakini kwa nini nitolewe na huku nikiwa ninahali nzuri ya mchezo na naweza kufanya vema zaidi" alisema Kiiza.
Kiiza hata hivyo hadi kufikia kumalizika kwa mzunguko huo wa kwanza wa ligi amemaliza huku akiwa na magoli nane huku Hamis Tambwe wa Simba akiwa na magoli 10.


No comments:

Post a Comment