YANGA
imemaliza mzunguko wa kwanza wa ligi huku ikiwa inaongoza ligi hiyo kwa pointi
28 huku ikiziacha timu za Azam Fc pamoja na Mbeya City zikiwa zote na pointi
27.
Katika
mchezo wa Uwanja wa Taifa Dar es salaam Yanga iliandika bao la kwanza kupitia
mchezaji wake Simon Msuva katika dakika ya 25
ya mchezo baada ya kuaptiwa pasi safi na Haruna Niyozima.
Dakika ya 30
mshambiliaji wa Yanga, Mrisho Ngasa aliachia shuti kali akiwa katikati ya
uwanja na kuandika bao la pili la timu hiyo.
Ngasa mnano
dakika ya 53 alioneshwa kadi ya njano kufuatia kumchezea vibaya mchezaji Amir
Omary.
Harakati za
Ngasa za kuongeza bao jingine zilizaa matunda katika dakika ya 56 baada ya
kutoa pasi safi iliyomkuta Jerryson Tegete ambae aliumalizia mpira huo uliomwacha
kipa wa JKT Oljoro Damas Kugesha akiwa chini.
Yanga
ilijitaidi kuendelea kutafuta magoli huku mchezaji wake Simon Msuva akiwa anaendeleza harakati za kufunga
lakini hata hivyo alipoteza pasi nyingi za mara kwa mara.
Kuna wakati
Msuva alishindwa kumalizia pasi ya wazi aliyopewa na mchezaji Jerryson Tegete.
Mchezaji
Niyozima alitolewa nje na kuingia Bahamuzi ambae nae iwapo angetumia vema
kufunga magoli nafasi alizokuwa akizipata huenda Yanga ingemaliza mzunguko huo
kwa 4-0.
Kuna wakati
Bahamuzi alibakia na kipa wa JKT Oljoro lakini hata hivyo shuti lake lilitoka
nje ya uwanja.
Amisi Kiiza
nae iwapo asingekuwa mchoyo wa pasi basi huenda angeiwezesha Yanga kupata mabao
mengi zaidi.
Uchoyo huo
wa pasi ndio uliopelekea kocha wa Yanga Ernest Brandits kumgtoa nje na kisha
kumuingiza Jerryson Tegete alieipatia Yanga bao la tatu.
Kutolewa kwa
Kiiza na kuingizwa Tegete kulimchukiza mchezaji huyo hadi alifikia hatua ya
kutoka kabisa nje ya benchi la ufundi na kwenda kukaa kwenye jukwaa la
mashabiki wa Yanga.
Wakati mechi
ilipoisha wakati wachezaji hao wakienda kwenye chumba cha kubadilishia nguo
huku wakiwa na mazungumzo na Mwenyekiti wao Yusuph Manji, Kiiza alitoka nje ya
chumba hicho huku akiwa amekasirika.
Kiiza
alienda hadi nje ya uwanja ambapo alisikika akizungumza na baadhi ya wapenzi wa
timu hiyo ambapo alikuwa akilalamikia hatua hiyo yakutolewa nje na kocha.
Kama
haitoshi aliendelea kulalama na kufikia hatua ya kusisitiza kuwa kocha huyo
alikuwa hampendi na ndio maana alimtoa huku akiwa bado ana hali ya mchezo.
" Mimi
ni mchezjai na mwenye uwezo lakini kwa nini nitolewe na huku nikiwa ninahali
nzuri ya mchezo na naweza kufanya vema zaidi" alisema Kiiza.
Kiiza hata
hivyo hadi kufikia kumalizika kwa mzunguko huo wa kwanza wa ligi amemaliza huku
akiwa na magoli nane huku Hamis Tambwe wa Simba akiwa na magoli 10.
No comments:
Post a Comment