Geoffrey Mutaiakifurahia baada ya kushinda mbio hizo
Mutai finished alimaliza ndani ya muda mfupi
Washindi wa kike Winner Priscah Jeptoo celebrates, na Buzunesh Deba na Jelena Prokopcuka (kulia)
Wanariadha wa Kenya Geoffrey Mutai na Priscah Jeptoo jana Jumapili wamenyakua ushindi wa taji la mbio za nyika huko New York City Marekani wakati vinara hao waliporejea katika mashindano hayo mwaka mmoja baada ya kimbunga cha Sandy kusababisha kuahirishwa kwa mbio hizo miezi saba baada ya shambulio la mabomu wakati wa mashindano ya Boston.
Mutai ambaye pia alishinda taji la mashindano ya New York mwaka 2011, ameibuka mshindi kwa uapande wa wanaume baada ya kumaliza mbio hizo kwa muda rasmi wa saa 2 dakika 8 na sekunde 24, akimtangulia mshindani mwenza Tsegaye Kebede wa Ethiopia kwa sekunde 52 lakini akirudi nyuma kwa rekodi aliyoiweka miaka miwili iliyopita.
Kwa upande wake Jeptoo bingwa wa mashindano ya London kwa upande wa wanawake ambaye alimaliza katika nafasi ya pili mwaka jana kwenye mashindano ya Olympiki huko London Uingereza,akitokea nyuma aliweza kushinda nafasi ya kwanza kwa kumaliza katika muda wa saa 2 dakika 25 na sekunde 7.
Makala ya 43 ya mbio hizo za umbali wa kilomita 42.2 lilihusisha zaidi ya wanariadha elfu 48 kutoka mataifa 115 yanayoshindania kitita cha dola laki moja huku usalama ukiimarishwa kufuatia
matukio mawili yaliyojitokeza awali katika mashindano hayo.
Priscah Jeptoo kutoka Kenya ndie aliyeshinda mbio hizo kwa upande wa wanawake mbio za New York City Marathon huko New York
Washindi wakipozi kupata picha ya pamoja hapa kwa upande wa mbio hizo kwa wanawake
usipime ilikuwa balaa!!!!
Tutafika tu!!
Wakikatiza juu ya daraja
A NYPD helicopter nayo ilikuwepo juu kucheki kama kunawatakao pata matatizo na hapa ilikuwa ikichunguza sehemu muhimu kwenye Daraja kama watapita salama wote.
No comments:
Post a Comment