Jurgen Klopp wakati wa mtanange wa kwanza Emirates ambapo timu yake ilishinda bao 2-1 dhidi ya Gunners na sasa kesho jumatano wapo kwake Dortmund.Arsenal wako Kundi F ambalo Vinara ni Borussia Dortmund wakifuatia Arsenal kisha Napoli lakini Timu zote hizi zina Pointi 6 kila mmoja na Marseille yuko mkiani akiwa hana hata Pointi.
Kocha wa Dortmund Klopp (kulia) amedai kuwa anaipenda Arsenal na anajua muziki wao hivyo timu yao haitawabeza hata kidogo na pia anamkubali mtu mzima mzee Arsene Wenger na amemuita 'Sir'
Mchezaji wa Borussia Dortmund akikwaana na Ozil wa Arsenal katika mechi ya kwanza ambapo kesho jumatano wanarudiana huko kwao Dortmund.
Klopp hivi karibuni amesaidi mkataba mpya wa kumuweka klabini hapo hadi mwaka 2018 na hivi karibuni aliongoza kikosi chake kikamnyuka mtu bao 6-1 dhidi ya Stuttgart ijumaa iliyopita.
Kocha Klopp akiwapongeza wachezaji wake baada ya kumfunga mtu bao 6-1 juzi ijumaa
Robert Lewandowski ndiye aliyefunga bao la pili wakati wa mtanange wa kwanza Emirates hivyo na kesho jumatano wenda akaongeza mabao hivyo Arsenal wajiandae kwa ukabaji
Gunners mpo hapo!!!
Klopp akiwa na midfielder wake Kevin Grosskreutz
Lewandowski mbele ya mashabiki wao wa Dortimund.
RATIBA YA MITANANGE YA KESHO JUMATANO.
Jumatano 6 Nov 2013
FC Basel 1893 v FC Steaua Bucureşti
Chelsea FC v FC Schalke 04
Borussia Dortmund v Arsenal FC
SSC Napoli v Olympique de Marseille
Football Club Zenit v FC Porto [Saa 2 Usiku]
Club Atlético de Madrid v FK Austria Wien
AFC Ajax v Celtic FC
FC Barcelona v AC Milan
RATIBA YA MITANANGE YA KESHO JUMATANO.
Jumatano 6 Nov 2013
FC Basel 1893 v FC Steaua Bucureşti
Chelsea FC v FC Schalke 04
Borussia Dortmund v Arsenal FC
SSC Napoli v Olympique de Marseille
Football Club Zenit v FC Porto [Saa 2 Usiku]
Club Atlético de Madrid v FK Austria Wien
AFC Ajax v Celtic FC
FC Barcelona v AC Milan
No comments:
Post a Comment