Pages

Saturday, November 30, 2013

UHAI CUP: FAINALI NI YANGA NA COASTAL UNION

 

 Kikosi cha pili cha vijana wa Jangwani Dar es Salaam Young African kimefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya Uhai kufuatia hii leo katika nusu fainali ya pili kuchomoza na ushindi mrefu wa mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo uliochezwa uwanja Azam Complex ulioko Chamazi.

Itakumbukwa jana Wagosi wa kaya Coastal Union ilifanikiwa kuwachapa waliokuwa mabingwa watetezi Azam fc katika nusu fainali ya kwanza kwa bao 1-0 kwenye uwanja huohuo wa Azam Complex.
 
Yanga na Coastal sasa zitakutana Jumapili hukohuko Chamazi kusaka bingwa wa michuano hiyo msimu huu ikiwa ni fainali ambayo inazirejesha uwanjani timu hizo ambazo zilikutana mapema katika hatua ya makundi ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
 
Itakumbukwa katika mchezo wa hatua ya makundi Novemba 19Coastal Union walikubali kufungwa bao 1-0 na vijana wa Yanga mchezo uliopigwa uwanja wa Karume Ilala jijini Dar es salaam.

Mechi hiyo iliyochezwa asubuhi saa mbili na kukamilika saa tatu na nusu, ilikuwa na ushindani mkubwa katika kipindi cha kwanza ambapo vuta nikuvute kati ya timu hizo ilikuwa kali, na hakukuwa na timu iliyotabiriwa kutoka kifua mbele kutokana na wote kucheza mchezo wa kujihami.
 
Coastal Union watakuwa wakimtegemeza zaidi nahodha wao Nzara Ndaro ambaye amekuwa kiunganishi mzuri wa kikosi ilhali yanga watakuwa wakimtegemea Hamis Issa ambaye aliwafunga Coastal katika mchezo wa hatua ya makundi.
 
Hii ni mara ya pili Coastal Union, wanashiriki michuano hiyo ya Uhai ambapo mwaka jana walifika mpaka hatua ya fainali wakatolewa kwa matuta na Azam FC.
 
Mechi ya fainali itatanguliwa na ile ya kutafuta mshindi wa tatu kati ya Azam na Mtibwa.

No comments:

Post a Comment