Pages

Saturday, November 30, 2013

MICHUANO YA CHALENJI: UGANDA YAIFUNGA RWANDA

Mshambuiliaji wa timu ya taifa ya Uganda Dan Sserukuma hii leo ameandika bao muhimu kwa kikosi cha kocha Milutin Sedrojevic Micho kufuatia kuandika bao pekee la dakika za majeruhi na kuipa Uganda ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya wanaodhaniwa kuwa sasa ndio wapinzani wao wakubwa timu ya taifa ya Rwanda maarufu kama Amavubi.
 
 Mshambuliaji huyo mjanja ambaye anachezea mabingwa wa soka nchini Kenya Gor Mahia alifanikiwa kuwazidi ujanja walinzi wa Rwanda waliovurugana na kuandika bao pekee kwa timu yake katika mchezo uliopigwa uwanja Nyayo jijini Nairobi.

Kufuatia ushindi huo wa Uganda ambao katika mchezo wa kwanza walikwenda sare ya bao 1-1 na wenyeji Kenya sasa watakuwa katika nafasi ya pili katika msimamo wa kundi C kutokana na Sudan kuwafunga Eritrea mabao 3-0 katika mchezo mwingine wa kundi hilo ulipigwa katika dimba la Machackos.

Mabao ya Sudan yamewekwa wavuni na Saleh Ibrahim kunako dakika 5 na 27 huku bao la tatu likiwekwa wavuni na Mohamed Taher dakika 34.

Vikosi
UGANDA CRANES:
Benjamin Ochan (gk), Nicholas Wadada, Godfrey Walusimbi ©, Richard Kasagga, Savio Kabugo, Aucho Khalid, Geoffrey Kizito, Hamis Kiiza, Mpande Joseph, Daniel Sserunkuma and Brian Majwega
 SUBS:
Ismael Watenga (gk), Said Kyeyune, Julius Ntambi, Martin Mpuga, Ibrahim Kizza, Vincent Kayizzi, Isaac Muleme and Franco Oringa.

RWANDA:
Ndayishimye Jean, Haruna Niyonzima, Nshutiyamagara Ismael, Bayisenge Emery, Ngirishuti Mwemere, Omberenga Fitina, Baptiste Mugiraneza, Meddie Kagere, Mushimiyimana Mohammad, Tuyisenge Jacques and Jean Claude Iranzi.
SUBS: Ndori Jean-Claude, Tubane James, Sibomana Abouba, Twagizimana Fabrice, Nduhukira Micheal, Rushenganga Michel and Mugabo Ciyan Hussein

No comments:

Post a Comment