Pages

Monday, November 11, 2013

TOURE, MOSES, OBI MIKEL, AUBAMEYANG, PITROIPA KATIKA KINYANG'ANYIRO CHA TUZO ZA BBC.

WACHEZAJI nyota watano kutoka Afrika wameteuliwa kugombea tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika, tuzo ambazo zinaandaliwa na shirika la utangazaji la Uingereza BBC. Wachezaji walioteuliwa katika tuzo hiyo ni pamoja na Yaya Toure wa Ivory Coast ambaye anatokea katika orodha hizo kwa mara ya tano, Victor Moses na John Mikel Obi wa Nigeria, Jonathan Pitroipa wa Burkina Faso na Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon. Mshindi wa tuzo hiyo atachaguliwa na mashabiki wa soka wa Afrika ambao watapata nafasi ya kupiga kura kutumia ujumbe mfupi wa simu zao mpaka Novemba 25 mwaka huu. Mshindi atatangazwa Jumatatu Desemba 2 kupitia kipindi cha radio na luninga cha BBC Focus on Afrika. 

No comments:

Post a Comment