Pages

Monday, November 11, 2013

DJOKOVIC NA NADAL KUKUTANA USO KWA USO KWENYE FAINALI YA DUNIA YA MICHEZO YA TENESI JIJINI LONDON.

Novak Djokovic amefanikiwa kumfunga Stanislas Wawrinka kwenye michuano ya dunia ya Tennes nchini Uingereza na kufikisha rekodi ya kushinda mechi 21mfululizo bila ya kupoteza na sasa kukutana na Rafael Nadal kwenye fainali. 
Djokovic ambaye anatetea ubingwa huo alifanikiwa kuchomoza na ushindi wa seti mbili bila kwa matokeo ya 6-3 na 6-3 dhidi ya Stanislas Wawrinka kwenye nusu fainali ya pili.
Djokovic alisubiri mpaka dakika ya mwisho kwenye seti ya pili kuweza kusmhinda mpinzani wake ambaye alionekana kummudu vema kiasi kilichowafanya mashabiki waamini kuwa huenda Novak angeshindwa. 

Kwa ushindi huu sasa Novak atakutana hii leo kwenye fainali ya michuano hiyo dhidi ya Rafael Nadal ambaye alifanikiwa kumshinda Roger Federer kwa seti mbili bila kwa matokeo ya 7-5 na 6-3. 
Federer amekuwa na msimu mbaya mwaka huu kwa kupoteza mechi nyingi anazokutana na Nadal pamoja na Djokovic kwenye michuano mbalimbali ambayo wamekutana.
Fainali hiyo inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mchezo wa Tennesi.

No comments:

Post a Comment