Pages

Sunday, November 10, 2013

TANZANITE YAREJEA NA MATUMAINI YA KUIFUNGA AFRIKA KUSINI

Kikosi cha Tanzanite na benchi la Ufundi baada ya kurejea nyumbani leo


Hapa wanapanda basi kuelekea kambini Msimbazi Centre

"Mama na Mwana" Mchezaji Sherda Bonifice anajua kuzifumania nyavu akiwa na mama yake. Kwenye michezo miwili ana mabao 6

Mzazi aka Kenedy Mwaisabula alikuwepo kuwalaki vijana

Baadhi ya wazazi waliokuja kuwalaki binti zao
TIMU ya Taifa ya wanawake U-20 “Tanzanite” imewasili leo saa 9.00 alasiri  kwa ndege ya LAM toka Msumbiji ikiwa na matumaini ya kuifunga Afrika Kusini kwenye mchezo wa raundi ya pili ya mashindano ya Kombe la Dunia yatakayofanyika nchini Canada mwakani.

Tanzanite iliyokwenda kucheza na wenzao wa Msumbiji na kufanikiwa kuwafunga mabao 5-1 hivyo kuwafanya kuaga mashindano hayo kwa mabao 15-1 baada ya mchezo wa awali kuifunga mabao 10-0 nyumbani.

Akizungungumza mara baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, kocha wa timu hiyo, Rogasian Kaijage alisema kuwa mchezo huo ulikuwa mgumu kiasi kwamba alilazimika kuwaambia wachezaji wake wacheze mchezo rahisi kutokana na kuhofia kuonyeshwa kadi.

“Nashukuru tumefuzu lakini hata wakati tunaondoka tuliwaahidi tunakwenda kufanya kile ambacho watanzania wanakipenda ila mchezo ulikuwa mgumu mpaka nikalazimika kuwaambia wachezaji wacheze mchezo rahisi (easy game)”, alisema Kaijage.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo ujao Kaijage alisema kuwa hategemei kufanya mabadiliko sana kwani timu yake ni nzuri na wachezaji wanajua wanatakiwa kufanya nini na kwa wakati gani hivyo atahakikisha kuwa anawajenga wachezaji kwenye utimamu wa mwili na akili pia.

Naye Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchin, Boniface Wambura, ambaye pia anakaimu nafasi ya Katibu Mkuu wa shirikisho hilo aliwapongeza wachezaji pamoja na benchi la ufundi kwa hatua waliyofikia na kuwa ahidi kuwatafutia michezo ya kirafiki ya kimataifa ili wajipime kwani wanapokwenda ni kugumu zaidi.

Mechi ya kwanza ya Tanzanite na Afrika Kusini itachezwa jijini Dar es Salaam kati ya 
Desemba 6 na 8 mwaka huu wakati ile ya marudiano itafanyika Afrika Kusini kati ya Desemba 20-22 mwaka huu.



No comments:

Post a Comment