Pages

Saturday, November 9, 2013

PIGUE: RONALDO ANAPATA MOTISHA KUTOKA KWA MESSI

BEKI mahiri wa klabu ya Barcelona, Gerard Pique amedai kuwa Cristiano Ronaldo anapata motisha kutoka kwa hasimu wake Lionel Messi hatua inayopelekea awe katika kiwango chake cha juu.
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid amekuwa akimaliza kama mshindi wa pili katika tuzo za Ballo d’Or katika kipindi cha miaka miwili iliyopita huku mwaka huu pia wakiwa katika kinyang’anyiro hicho. Pique ambaye alicheza kwa kipindi kifupi Manchester United anafikiri Ronaldo mwenye umri wa miaka 28 anapata nguvu za kujituma zaidi kutoka kwa Messi na kumsifu nyota huyo ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Ureno kwa juhudi zake hizo. Pique amesema Ronaldo hajabadilika toka wakiwa wote United, ni mchezaji ambaye anamuhusudu kwasababu anafanya kazi kwa bidii kuwepo hapo alipo.
LA LIGA
RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Novemba 8 

Granada CF 3 v Malaga CF 1
Osasuna 0  v Almeria 1

Jumamosi Novemba 9 
18:00 Real Madrid v CF Real Sociedad
20:00 Getafe v Elche
22:00 Athletic de Bilbao v Levante
00:00 Celta de Vigo v Rayo Vallecano

Jumapili Novemba 10
14:00 RCD Espanyol v Sevilla FC
19:00 Valencia v Real Valladolid
21:00 Villarreal v Atletico de Madrid
23:00 Real Betis v FC Barcelona

No comments:

Post a Comment