Pages

Saturday, November 9, 2013

MCHEZO WA MARUDIANO KATI YA AL AHLY NA ORLANDO PIRATES KUPIGWA KESHO SAA MOJA, NANI KUIBUKA KIDEDEA


JUMAPILI Usiku huko Cairo Nchini Egypt Klabu Bingwa ya Afrika itapatikana baada ya Mechi ya Marudiano ya Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI kati ya Mabingwa Watetezi Al Ahly ya Egypt na Orlando Pirates ya Afrika Kusini huku Al Ahly wakiwa na hazina ya Bao la Ugenini kwani Timu hizi zilitoka Sare ya Bo 1-1 huko Johannesburg Wiki iliyopita. 
Katika Mechi hiyo ya kwanza Al Ahly walitangulia kufunga kwa Bao la frikiki ya Mkongwe Mohamed Aboutrika katika Dakika ya 14 na Pirates kusawazisha kwa Bao la mwishoni la Dakika za Majeruhi la Thabo Matlaba.
Timu hizi pia zilikuwa kwenye Kundi moja kwenye Mashindano haya na Pirates kuifunga Al Ahly 3-0 huko Egypt kwenye Mechi ambayo walidai kipigo hicho ni kwa sababu walikuwa kwenye Mfungo wa Ramadhani. 

Katika Marudiano huko Johannesburg, Pirates na Al Ahly zilitoka 0-0 na zote hizi kufuzu kuingia Nusu Fainali.
Kwenye Nusu Fainali, Pirates waliibwaga Esperance ya Tunisia kwa Bao la Ugenini baada kutoka 0-0 huko Johannesburg na 1-1 huko Tunis.
Nao Al Ahly walitoka 1-1 na Coton Sport ya Cameroun katika Mechi zao zote mbili na Al Ahly kutinga Fainali kwa Mikwaju ya Penati 7-6. 

Wakati Orlando Pirates wametwaa CAF CHAMPIONZ LIGI mara 1 tu, Mwaka 1995, Al Ahly washabeba Ubingwa huu mara 7.
Mechi hii ya Marudiano itaanza Saa 1 Usiku kwa Saa za Bongo na kurushwa moja kwa moja na Kituo cha TV cha SuperSport.
Timu hizi zitarudiana Jumapili ijayo huko Cairo na Mshindi atakuwa Klabu Bingwa ya Afrika ambayo itacheza Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani Mwezi ujao huko Morocco.
Mchezaji Veterani wa Al Ahky, Mohamed Aboutrika, ndie aliewapa Mabingwa hao wa Afrika Bao lao kwa frikiki ya Dakika ya 14.
Lakini Thabo Matlaba alisawazisha kwa Pirates katika Dakika ya 3 ya Dakika za Nyongeza baada Dakika 90 kumalizika.
 Mshindi wa mchuano huo ataliwakilisha bara la Afrika katika michuano ya dunia ya klabu bingwa, itakayofanyika kati ya tarehe 11 hadi 21 mwezi ujao nchini Morroco.

VIKOSI VINATARAJIA KUWA HIVI:-
AL AHLY
Ekramy
Fadil, Gomaa, Naguib, Moawad
Fathy, Ashour
Soliman, Aboutreika, El Said
Zaher 


ORLANDO PIRATES
Meyiwa
Lekgwathi, Gcaba, Mahamutsa, Matlaba
Manyisa, Masalesa,
Klate, Myeni, Segolela
Bacela

No comments:

Post a Comment