Pages
▼
Saturday, November 16, 2013
NIGERIA YAKATA TIKETI YA KOMBE LA DUNIA BAADA YA KUINGA ETHIOPIA 2-0
TIMU ya taifa ya Nigeria imekuwa nchi ya kwanza ya Afrika kukata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwakani baada ya ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Ethiopia leo.
Victor Moses alifunga kwa penalti dakika ya 20 na Victor Obinna akaongeza la pili dakika ya 82 kwa mpira wa adhabu, hivyo Super Eagles kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 4-1, baada ya awali kushinda 2- mjini Addis Ababa mwezi uliopita katika mchezo wa kwanza.
Nigeria inafuzu kwa mara ya tano kucheza Fainali za Kombe la Dunia, ambazo mwakani zitafanyika nchini Brazil, baada ya awali kucheza fainali nne zilizopita.
Mechi nyingine nne za kufuzu kwa fainali hizo barani zitakamilika ndani ya siku nne wayi mchezo mwingine wa leo ni kati ya Senegal na Ivory Coast.
No comments:
Post a Comment