Pages

Tuesday, November 26, 2013

MBABE WA MASUMBWI MANNY PACQUIAO KUTEMBELEA MJI WA TACLOBAN BAADA YA KUKUMBWA NA KIMBUKA KIKALI TYPHOON HAIYAN!!

Mwana masumbwi Manny Pacquiao ameahidi kutembelea maeneo yaliyoathiriwa vibaya na kimbunga Haiyan nchini Ufilipino hasa kwenye mji wa Tacloban siku chache zijazo baada ya kutetea ubingwa wake.
Mashindano ya kimataifa ya ngumi za uzani wa kati yametangazwa jana Jumapili kwenye vituo vinne vya wazi mjini Tacloban ili kuwatia moyo wakazi wa maeneo hayo baada ya kukumbwa na kimbunga kilichoathiri maisha yao.


Katika mashindano hayo mbunge Pacquiao akaibuka mshindi dhidi ya mpinzani wake Brandon Rios kwa raundi 12 huko Maca ,na kutangaza kuwa kipaumbele chake ni kutembelea mji wa Tacloban kama alivyowaahidi wakazi wa mji huo.

Pacquiao ameongeza kuwa timu yake inashughulikia kupata taarifa zitakazo mwezesha kusafiri hadi kwenye mji mkuu wa jimbo la Leyte na atakuwa huko ndani ya siku chache zijazo.







Kijana wa Filipino akikatiza kwenye mtaa ambao umeharibiwa vibaya na kimbuga kikali kwenye mji wa Tacloban huko Philippines.

No comments:

Post a Comment